TRA

TRA

Latest

Friday, March 23, 2018

Hospitali Mashua ndani ya Ziwa Victoria yahudumia Wagonjwa 55,600 mwaka 2017

No comments:

 

HOSPITALI ya  Mashua ndani ya Ziwa Victoria ni jitihada za Taasisi ya Jubilee Hope Medical and Dental Programme, ambayo imetibu zaidi ya wagonjwa 55,600 kwa mwaka 2017, ikiwa ni mafanikio makubwa katika historia ya Miradi ya Binadamu.
Tangu kuanzishwa kwa Mradi huo miaka minne iliyopita, Jumla ya Wagonjwa 158,000 wamepatiwa huduma hiyo.
Ninashukuru sana kuletwa kwa huduma hii kwenye kisiwa chetu,” alisema Bi Asha Ruhenga, Mkazi wa Kisiwa cha Chakazimbwe. “Kwa kuwa huduma hii ya Afya ni nadra kwenye Jamii yetu,kila itokeapo kuna matangazo kuwa mashua hiyo itatia Nanga, sehemu kubwa ya Jamii hujitokeza.”
Jitihada katika Mradi huu zinahusisha Kanisa la African Inland Church Tanzania, Taasisi ya Vine Trust kutoka Scotland pamoja na Geita Gold Mining Limited (GGML) ambapo kwa pamoja hutoa huduma ya Msingi ya Afya kwa wakazi 450,000 waliopo ndani ya Visiwa vya Ziwa Victoria.
Mgodi wa Dhahabu Geita (GGML) huchangia gharama ya matengenezo, mafuta na vilainishi katika kuisaidia mashua hiyo kuhudumia wagonjwa.
Hospitali Mashua hutoa huduma mbalimbali zikiwemo Elimu, Upimaji Afya wa Jumla, Matibabu ya mama na mtoto, Chanjo, Huduma ya uzazi, Afya ya Meno, Upimaji hiari wa UKIMWI pamoja na utoaji nasaha,
Vile vile Mashua hiyo hutoa huduma ya Maabara pamoja na huduma za jumla za famasia bure bila gharama yoyote.
"Tunajivunia kuwa, kwenye mwaka wake wa kwanza wa ufunguzi wa huduma hii, Hospitali Mashua ilifikia jumla ya Watu 46,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto waishio ndani ya visiwa vya Ziwa Victoria ambavyo vina changamoto kubwa ya kupata huduma ya Afya kutokana na umbali,” alisema Mchungaji Samuel S. Limbe, Katibu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania Wilaya ya Geita.
Na kwa mwaka jana pekee, zaidi ya Wagonjwa 55,600 walinufaika na huduma ya Mashua hiyo, jambo linalodhihirisha uhitaji mkubwa wa huduma ya Afya kwenye visiwa hivyo.”
Mashua Hospitali hiyo hufanya mzunguko wake ndani ya Visiwa vya Ziwa Victoria kwa majuma mawili na baadaye kurudi jijini Mwanza kwa ajili ya matengenezo, Kuongeza Vifaa Tiba na kujaza mafuta kabla ya kurejea tena kutoa huduma ya Afya ndani ya Visiwa hivyo.
Hii ni Mashua ya kwanza ya aina yake kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. “Tunafarijika kuwa sehemu ya jitihada hizi zilizotukuka za kutoa huduma ya Afya kwa Wagonjwa na wenye uhitaji ndani ya Visiwa vya Ziwa Victoria,” alizungumza Makamu wa Rais wa Miradi Endelevu kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita Bw Simon Shayo.
Tunahitaji watu wenye Afya bora katika kutuletea maendeleo ya Uchumi na maendeleo ya Jamii.”

Wednesday, March 14, 2018

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO MACHI 14, 2018

No comments:

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger