TRA

TRA

Sunday, January 31, 2016

Mkoa wa Dar es Salaam Sasa Kuwa na Wilaya Tano

No comments:



RAIS Dk. John Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano

VIDEO.....RAIS MUGABE AMCHANA LIVE BAN KI MOON MBELE YAKE ..AMTAJA KIKWETE NA CCM PIA .

No comments:


MAGAZETI YA LEO JUMATATU

No comments:

























MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA MASUALA YA USALAMA BARANI AFRIKA.

No comments:

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO lenye makamo makuu yake Nchini Vienna Ausria Bw. Li Yong walipokuta katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa leo Januari 31,2016, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa lenye Makao Makuu yake Nchini Vienna Austria uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Li Yong, leo Januari 31,2016 kwenye Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, katika mazungumzo yao Viongozi hao walizungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya Viwanda utakaotolewa na UNIDO kwa Serikali ya Tanzania ili kuifanya Tanzania iwe Nchi ya Viwanda kuanzia mwaka 2015/2020, ambapo Mkurugenzi huyo ameahidi kuitembelea Tanzania wakati wowote kuanzia sasa. Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea taarifa yenye mipango ya Maendeleo ya Viwanda kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa Bw. Li Yong baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo Januari 31,2016 katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.(Picha na OMR)

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amtembelea Rais Mstaafu Mkapa.

No comments:

 
Picha mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa. Rais Dkt. Magufuli alikwenda kumsalimia Rais mstaafu Mkapa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Picha na IKULU.

JAJI MKUU MHE MOHAMED CHANDE .OTHMAN AFUNGUA RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI MWAKA 2016

No comments:


Watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa maandamano leo jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari wa Jeshi la Magereza na Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiwa wamebeba mabango ya Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es salaam.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.


Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (katikati) akiongoza mazoezi ya pamoja ya Wadau wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria nchini.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  akizungumza na wadau mbalimbali wa Mahakama waliohudhuria Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam.


Baadhi ya Wanachi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini leo jijini Dar es salaam. Wengine katika picha ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kutoka kushoto).


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Watendaji wa Mahakama, Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria leo jijini Dar es salaam.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo katika viwanja vya Mnazi Mmmoja wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu ( wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila ( wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya  Watendaji na Watumishi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Msajili wa Mahakama, Wakuu wa Idara  na Vitengo wa Mahakama ya Tanzania leo wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa tatu kutoka kushoto).


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Jeshi la Magereza leo wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Mahakama ya Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Watumishi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).

MAJALIWA AHUDHURIA IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI MKUU WA KKKT TANZANIA ASKOFU SHOO MJINI MOSHI.

No comments:


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea picha aliyopewa na Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli,Askofu Frederck Shoo katika ibada ya kumuingiza kazini askofu huyo ilyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Baadhi ya waalikwa walioshiriki katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Wachina waishio nchini waadhimisha mwaka mpya 2016 wa "Ngedere"

No comments:


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akifungua Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni mshereheshaji ajiyejitambulisha kwa jina la “Sharobaro”.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Salim Ahmed Salim (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kulia) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (katikati) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim  Dkt. Ahmed Salim na kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
 Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) na Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) wakisalimiana wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
 Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Salim Ahmed Salim (kulia) na Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) wakisalimiana wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
 Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya raia wa Kichina wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya raia wa Kichina wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya raia wa Kichina wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya michezo iliyooneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya michezo iliyooneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya michezo iliyooneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akichanganya tiketi za bahatinasibu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
  Fashifashi na fataki  zilizowashwa kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Fashifashi na fataki zilizowashwa kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Fashifashi na  fataki zilizowashwa kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO
 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger