Kaimu Katibu Mkuu uvccm Taifa SHAKA HAMDU SHAKA akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wilaya ya Mwanga
Kaimu katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akifungua shina la wakereketwa wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a
kikundi cha ngoma kutoka katika kabila la kichaga kikitumbuiza wakati wa kaimu katibu mkuu wa UVCCM akiwasili wilayani Mwanga
Na Woinde Shizza, Mwanga
Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umewataka wananchi wa mikoa ya
Kaskazini mwa Tanzania kukataa na kuzikwepa siasa za uzawa na ukanda
kwasababu ubaguzi ni dhambi isiyosamehewa na mungu.
Wametakiwa
kutambua kuwa ubaguzi ni zaidi ya laana ambayo ikiemea na kujengeka
katika jamii kuiondosha kwake ni kazi ngumu na kwamba kafara yake
lazima maisha ya watu yapotee au damu imwagike.
Hayo
yameelezwa leo na Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu shaka wakati
akizungumza na wanachama wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a kata ya
Mwanga mkoani hapa.
Shaka alisema ni aibu binadamu
aliyestaarabika, kupata elimu akawa anaishi, kupigania madaraka., vyeo
au utawala kwa kutumia maneno au sera za ubaguzi wa dini, ukabila,
uzawa au ukanda.
Aidha aliongeza kuwa baada ya miaka 52 ya
uhuru na Muungamo wa mataifa ya Tanganyika na zanzibar, anapotokea
kiongozi au chama cha siasa kinachofanya shughuli za kisiasa kwa kueneza
sumu ya uzawa na watu kupiga kura kwa ukanda ni hatari mpya mbele ya
watanzania.
"Ndugu zangu wananchi wa mikoa ya Kaskazini kuna
hatari inawanyemelea, msipoitahadhari na kukwepa, ikiwaingia kutoka
kwake ni mbinde, ili ifanyike kafara ya kuondoa laana hiyo si ajabu
damu ikanwagika "alisema Shaka
Alisema wakati baadhi ya
wananchi wa mikoa hiyo wakiaza kughilibiwa na wanasiasa uchwara wakubali
kuchagua vyana kwa sababu za ukanda na ukabila, idadi kubwa ya wakaazi
wa Mikao hiyo wanaishi na wamejijenga kiuchumi katika mikoa mingine ya
nchi na huko hawabughudhiwi wala kubaguliwa.
"Haiikisha
mkiendela kubagua wenzetu na nyinyi mtaanza kubaguliwa,vdhambi ya
ubaguzi haina toba, kataeni siasa chafu na wakwepeni matapeli wa kisiasa
na walafi wa madaraka "alisisitiza shaka.
Kaimu huyo katibu
mkuu wa UVCCM alisema kwamba Taifa la Tanania halikuachwa na wakoloni
bali liliundwa na waasisi wake Marehemu baba wa Taifa Mwalimu julius
Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume bila na kupiga vita ubaguzi wa
kikabila, udini, rangi za watu au kuendekeza uzawa.
Alisema
kutendo chochote kitakachopelekea kuacha au kuipuuza misingi ya Taifa
letu ambayo imewafanya watu kuwa na umoja, upendo na mshikamano
radhi za waasisi hao pamoja na za wenzao zitaigeukia nchi yetu iwapo
tutakubali kugawanywa na wanasiasa wachovu.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma alisisitiza haja
ya kuendelea kuheshimu na kudumisha umoja wa kitaifa nchini na
mwanasiasa yeyote atakayeonekaa kana ni mkabila, mdini na asiyehimiza
amani na utulivu aogopwe kama ebola.
"Ni mkoa upi leo hii nchini
kwetu ambao wanaishi janii ya watu wa kabila moja,dini moja,rangi moja
au ukoo mmoja,tikate ukabila ns vyama vilivyoanza kuonyesha ubaguzi wa
aina yeyote "alisema Raibu
Mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoani
kilimanjaro alisema vyama vinavyopita na kueneza siasa za chuki, ukanda
au ukabila vichunguzwe na ikiwa vitatjibiiyika kujihusisha na vitendo
hivyo hatari Msajili wa Vyama vya siasa nchini achukue hatua za
kisheria kuifuta mara moja kabla havijaleta madhara.
Shaka na msafara wake wanaendelea na ziara katika wilaya ya Mwanga kabla ya kuhitimisha wilaya ya Same baadae kuelekea
Mkoani Tanga.