Sunday, July 31, 2016
RAIS WA SIMBA, AVEVA AKITANGAZA MKUTANO KURIDHIA KUFANYA MABADILIKO
Chanzo Mo Blog
Hatimaye
ile ndoto ya mashabiki wa klabu ya Simba kuona klabu yao ikibadili
mfumo unaotumika sasa wa wanachama ndiyo kuwa wamiliki wa klabu na
kuingia katika mfumo wa kampuni imekamilika.
Hilo
limethibitishwa na Rais wa Simba, Evans Aveva katika mkutano mkuu wa
Simba ambao ulikuwa unafunga msimu wa 2015/2016 kwa kutolewa taarifa na
kuweka mipango mipya kwa msimu ujao.
Hatua
hiyo imekuja baada ya mmoja wa mashabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji
na Rais wa makampuni ya Mohammed Enterprises, Mohammed Dewji “MO”
kutangaza nia ya kutaka kununua hisa za asilimia 51 na kutoa Bilioni 20
kwa ajili ya kuisaidia Simba kurudi katika makali yake ikiwa ni pamoja
na kusajili wachezaji wazuri, kocha mzuri, kujenga kiwanja, kuweka vituo
vya kukuzia vipaji vya Simba na vingine vingi.
Kutokana
na jambo hilo, mashabiki wa Simba walionekana kuvutiwa na mipango ya MO
na hivyo kuandamana katika ofisi za klabu na kushinikiza uongozi
kukubaliana na MO ili kununua hisa na kuanza kuwekeza ili Simba irudi
katika makali ya kushinda mataji.
Ipo hapa video ikimuonyesha Rais wa Simba, Evans Aveva akitangaza mkutano wa Simba kuridhia kufanya mabadiliko.
RADIO MARIA WAIOMBA SERIKALI KUREKEBISHA SHERIA YA LESENI YA REDIO ZA JAMII
Mwashamu
Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara akikata keki wakati wa sherehe za
kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania jana Jijini
Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, katikati ni Mkurugenzi wa Redio
Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendejana.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akikata keki wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya
Redio Maria Tanzania jana Jijini Dar es Salaam yaliyoanza rasmi tangu
April 26 mwaka huu. Katikati ni Mwashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki
la Mtwara Titus Mdoe,kutoka kulia ni Mhamasishaji Mkuu wa Redio Maria
Tanzania Bi. Veronica Mwita na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Redio
Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendejana.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Benjamin William Mkapa akisalimiana na Baba Askofu wa Jimbo
Katoliki la Mtwara Mwashamu Askofu Titus Mdoe wakati wa sherehe za
maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania jana Jijini Dar es
Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padre. John
Maendejana.
Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Saalam Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo akizungumza na wadau na marafiki wa Redio Maria Tanzania jana
Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea
kuanzishwa kwa Redio hiyo
Mkurugenzi
wa Redio Maria Tanzania Padre John Maendeleo akizungumza na wadau na
marafiki wa Radio Maria Tanzania jana Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Rais wa
Redio Maria Tanzania Humphrey Julius Kira akizungumza na wadau na
marafiki wa Radio Maria Tanzania jana Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akipokea risala kutoka kwa Rais wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius
Kira(Kulia) wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya
Redio Maria Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akipeana mkono na baadhi ya marafiki wa Redio Maria Tanzania waliofika
kuchangia Redio hiyo katika harambee iliyofanyika ikiambatana na sherehe
za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania jana Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Rais wa Redio Maria Tanzania Bw. Humphrey Julius
Kira.
Baadhi ya waumini wa Roman Katoliki wakifurahi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania (RMTZ). Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Rais
wa Redio Maria Tanzania, Humphrey Kira ameiomba Serikali kurekebisha
Sheria ya leseni ya redio za jamii ili ziweze kuwa na vituo vingi vya
kurushia matangazo yake.
Hayo
yamesemwa jana na Rais huyo wakati alipokuwa akisoma risala kwenye
sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya redio hiyo
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Msimbazi Centre, Jijini Dar es Salaam.
Kira
amefafanua kuwa redio za kijamii hasa zilizojikita katika nyanja za
kiimani zinasaidia kufundisha maadili na kufanya wananchi wakomae
kiimani, hivyo angefurahi sana kuona redio za aina hiyo zinapewa leseni
za kurusha matangazo yake nchi nzima.
“Ndugu
mgeni rasmi, redio yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni
pamoja na ufinyu wa sehemu za usikivu (coverage areas) ambapo tatizo
hili linatokana na sheria ya leseni za redio ambayo hairuhusu redio za
aina hiyo kuwa na vituo zaidi ya kumi nchini nzima, tunaomba serikali
itusaidie kuiboresha sheria hii ili tuongeze vituo vya matangazo ya
dini”, alisema Kira.
Rais
huyo ameongeza kuwa majimbo yote yanahitaji kufikiwa na huduma za
maombi, hivyo anawashauri wasikilizaji wote kuendelea kuisikiliza redio
hiyo kwa njia ya mitandao ikiwemo simu za mkononi kwani hivi sasa huduma
hiyo inapatika nchi nzima.
Kwa
upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa rai kwa uongozi wa redio hiyo
kutobadilisha maudhui wala kuweka vipindi visivyokuwa vya dini ili
iendelee kuunganisha familia na sio kuzigawa familia.
“Tunasema
kuwa redio Maria ni sauti ya kikristu nyumbani mwako lakini mimi nasema
ni sauti ya Mungu ndani ya familia kwa kuwa inafanya kazi ya
kuunganisha familia, vyombo vingine vya habari vinafanya kazi kubwa ya
kuigawa familia lakini Redio Maria ni tofauti”, alisema Pengo.
Askofu
Pengo amewashukuru wananchi wote waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo
kwa kuwa kufanya hivyo ni njia moja wapo ya kumuenzi na kumpa heshima
Mama Bikira Maria.
Nchini
Tanzania, Redio Maria ilianzishwa Aprili 26 mwaka 1996 katika Jimbo Kuu
Katoliki la Songea ikiwa na lengo la kumsaidia Mama Bikira Maria katika
kazi yake ya kumtangaza Yesu Kristo kwa watu wote. Mpaka sasa ina vituo
10 Tanzania Bara na viwili Zanzibar. (P.T)
RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MKUTANO TINDE, ISAKA NA KAHAMA MKOANI SHINYANGA
Rais wa
Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi
wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea Nzega mkoa Tabora.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza jukwaani wimbo wa
kwaya ya Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT-Usharika wa Yeru Ndala
Shinyanga kabla ya Kuhutubia mamia ya wakazi Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa
zamani wa Kahama James Lembeli mara baada ya kuwasalimia wananchi
waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais katika viwanja hivyo vya Kahama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Isaka mkoani Shinyanga.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge
wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa Chadema mara
baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza pamoja na
Wanakwaya wa Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT-Usharika wa Yeru Ndala
Shinyanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano Kahama mjini mkoani
Shinyanga.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya
kuoneshwa picha na kijana mmoja aliyeishika picha hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Tinde mkoani Sinyanga.
PICHA NA IKULU (P.T)
ESRF YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUICHAMBUA BAJETI YA SERIKALI KATIKA SEKTA YA AFYA NA VIWANDA
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi
Kida, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mdahalo uliolenga kujadili changamoto
zinazoikabili bajeti ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Afya na
Viwanda, kwenye makao makuu ya ESRF jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo
umewakutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi. (Picha
zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said).
TAASISI ya Utafiti ya Uchumi na Jamii (ESRF)
imewakutanisha wasomi na wawakilishi wa taasisi za umma na kibinafsi
kuchambua bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Sekta ya Afya na
Viwanda ili kuona inavyoweza kutatua changamoto zinazokabili Sekta hizo
kwenye mdahalo uliokutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na
Binafsi na kufanyika makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Akifungua
mdahalo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt.Tausi Kida
alisema, Taasisi yake imeona ni vema kuwakutanisha wadau kujadili bajeti
hiyo katika sekta ya Afya na Viwanda, kwa vile zinagusa uchumi wa
wananchi.
Akiwasilisha
mada juu ya bajeti ya Serikali 2016/2017na changamoto zinazoikabili
sekta ya Afya, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi
Shirikishi, Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja alisema,
ingawa bajeti iliyotengwa kwenye sekta ya Afya ni kubwa, lakini bado
kuna changamoto kadhaa kwa vile Wizara hiyo imepanuka kutokana na
kuhudumia maeneo mengi.
Profesa
Mujinja alitolea mfano wa ununuzi wa madawa ambapo, zaidi ya asilimia
90 ya madawa yanayotumika huagizwa kutoka nje na hivyo fedha nyingi za
kigeni hutumika.
Katika
majumuisho yake, Profesa Mujinja alisema, ni vema Serikali ielekeze
nguvu zake kwenye uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha madawa na vifaa
tiba hapa nchini ili kwenda sambamba na malengo ya taifa ya maendeleo
endelevu.
Akizungumzia
kuhusu changamoto za bajeti kwenye eneo la Viwanda, muwasilisha mada
Profesa Prosper H. Ngowi kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es
Salaam, alisema, fedha zilizotengwa kwenye Sekta ya Viwanda ni Shilingi
Bilioni 81, 871,992,000, ambapo asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya
kawaida na asilimia 49 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Kwa
mtazamo wake, Profesa Ngowi alisema, mgawanyo huo ni mzuri na sio kwa
kiwango kikubwa kwani hakuna tofauti na bajeti ya mwaka 2015/2016, na
kuonyesha wasiwasi wake muda ambao Serikali inatoa fedha hizo kuhudumia
maeneo yaliyokusudiwa.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Cha
Muhimbili, Profesa Phares Mujinja, akitoa mada juu ya changamoto
zinazoikabili bajeti ya Serikali ya 2016/2017 kwenye Sekta ya Afya
wakati wa mdahalo huo.
“Bajeti
ya 2016/2017 ni Asilimia 70.3% ya ile ya 2015/2016 na kwamba wizara
hivi sasa ni kubwa kutokana na kuongezeka kwa sekta ya Uwekezaji.”
Alifafanua. (P.T)
WAZIRI NAPE AONGOZA KUAGA MWILI WA MPIGAPICHA MKONGWE JOSEPH SENGA, JIJINI DAR
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye akitoa heshima kwenye mwili wa marehemu Joseph Senga, Sinza jijini Dar es Salaam, jana
Naibu Wazri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia wambura akitoa heshima kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga jana Sinza Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania taima alilokuwa akifanyia kazi Joseph Senga, akitoa heshima mwa mwili wa marahemu Joseph Senga. Wafuatao ni waombolezaji wengine wakitoa heshima kwa mwili wa marehemu Joseph Senga
Subscribe to:
Posts (Atom)