TRA

TRA

Monday, October 31, 2016

Mkurugenzi wa FBI matatani

No comments:


Bildkombo James Comey und Hillary Clinton (Getty Images/AFP/Y. Gripas/J. Sullivan)
Seneta wa juu kabisa wa chama cha Democrat, amesema Mkurugenzi wa FBI James Comey anaweza kuwa amevunja sheria kwa kutangaza kubaini barua pepe mpya zinazoweza kuwa muhimu kwa uchunguzi dhidi Hillary Clinton
Katika barua yake kwa Comey, kiongozi wa kundi la wachache Harry Reid, seneta wa Nevada amemtuhumu kiongozi huyo kwa kuwa na undumilakuwili kwa kuwa na nia ya kudhibiti wito wa Democrat kujadili kile kinachoelezwa kuwa uwezekano wa mahusiano kati ya Donald Trump na serikali ya Urusi, na badala yake Ijumaa iliyopita kutoa taarifa kwa bunge la Marekani-Congress za ujumbe wa kingono, katika uchunguzi wa Anthony Weiner, mbunge wa zamani wa New York na mume wa zamani wa msaidizi wake mkuu wa Clinton Huma Abdidin.
Katika taarifa hiyo Reid amemwambia kiongozi huyo wa FB kuwa jitihada za wazi kabisa zenye kuonesha ana nia ya kusaidia upande mmoja wa chama. Aidha ameongeza kuwa ofisi yake imemuandikia barua hiyo kwa kutanabaisha kuwa amekiuka sheria iitwayo "Hatch Act", ambayo inawazuia maafisa wa FBI kutumia mamlaka yao ya kiofisi katika kufanikisha ushawishi katika chaguzi. Amesema kwa kitendo cha kujiegemeza kwa upande wa chama amevunja sheria za taifa hilo.
Kutikisika mbio za Ikulu ya Marekani
Comey amezitikisa mbio za ikulu ya Marekani- White House kwa barua yake kwa Congress, akiwaeleza wabunge kupatikana kwa barua pepe mpya. Chama cha Democrat kina wasiwasi uvumbuzi huo mpya unaweza kumpa nguvu mpya mgombea wa Republican katika juma la mwisho kuelekea uchaguzi wa rais pamoja na kuwaongezea nguvu wagombea wa useneta na baraza la wawakilishi katika uchaguzi huo.
Katika hatua tofauti kufuatia kadhia hiyo mwanasheria mkuu wa zamani Eric Holder na waendesha mashitka wengine kadha wa kadhia wametia saini barua inayomkosoa Comey kutokana na kisa hicho cha hivi karibuni cha namna anavyoshughulikia tuhuma za barua pepe za mgombea Clinton.
Katika barua hiyo ambayo shirika la habari la Ufaransa la AP imeipata nakala yake inasema Comey amejitenga na kitenmgo cha sheria pale alipolidokeza bunge la Marekani juu ya uchunguzi mpya wenye kuhusiana na uchunguzi mpya kuhusiana na kashfa ya Clinton.
Aidha barua hiyo vilevile imeeleza maafisa wa Kitengo cha Sheria nchini humo wameagizwa wasiendelee kujadili uchunguzi unaondelea na kujitenga kabisa na jambo hilo katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, kwa lengo la kuondosha ushawishi wao. Lakini mkurugezi wa FBI alikwisha sema pale alipozungumza na maafisa wenzanke wa shirika hilo la ujasusi Ijumaa iliyopita kuwa barua yake kwa bunge la Marekani ipo katika hatari ya kutoeleweka katika kipindi hiki cha karibu na uchaguzi, lakini alipsawa kulipa taarifa bunge hilo baada ya awali kulieleza kuwa uchguzi wake ulifungwa. DW

UHURU KENYATTA AMUANDALIA DHIFA YA KITAIFA MGENI Wake DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

No comments:



k1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.
k2
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Nairobi.
k3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigonganisha glass na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.
k4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margaret Kenyatta katika dhifa hiyo.
k5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo huku akiwa amewashika mikono kwa pamoja Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya William Ruto na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margaret Kenyatta katika dhifa hiyo ya kitaifa.
k6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mabalozi mbalimbali wa Kenya waliohudhuria katika dhifa hiyo ya Kitaifa.
PICHA NA IKULU (P.T)

TANZANIA YANG’ARA MAONYESHO YA BIASHARA NA UTALII SAUDI ARABIA

No comments:




Balozi Hemed Mgaza, wakati anaapa baada ya kuapishwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia.
Na Mwandishi Wetu, Saud Arabia
MAONYESHO ya biashara na Utalii yaliyoandaliwa nchini Saud Arabia katika Mji wake Mkuu wa Riyadh, yamefanyika wiki iliyopita huku Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikionekana kung’ara baada ya wageni wengi kupendezwa na bidhaa zilizokuwa zinaonyeshwa katika banda la Tanzania.
Katika maonyesho hayo ambayo bidhaa mbalimbali zilionyeshwa ukiwamo eneo maalum la mlima Kilimanjaro, nguo za Kitanzania na viatu pamoja na bidhaa nyingine muhimu zilizoonekana kuwapendeza wengi waliohudhuria maonyesho hayo.

Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Mheshimiwa Hemed Mgaza, alisema kwamba wananchi wengi waliohudhuria maonyesho hayo walionekana kuvutiwa zaidi na nchi ya Tanzania kutokana na vivutio vyake.
Alisema hali hiyo imekuja kutokana na aina ya bidhaa zilizoonyeshwa pamoja na ubunifu wa kutangaza bidhaa zao na nchi kwa ujumla, wakiamini kuwa utachochea wageni wengi wa kutoka nchini hapa kwenda kutembelea nchini Tanzania kwa mambo mbalimbali.

“Binafsi nimefarijika mno kutokana na wenyeji kuandaa maonyesho haya na kutuaalika Watanzania ambao watumishi wa ofisi yangu pamoja na mimi mwenyewe wote tulihakikisha kwamba tunayatumia vizuri kutangaza nchi yetu Tanzania.
“Tumewahakikishia kwamba mbali na nchi yetu kujawa na vivutio vingi kutoka Tanzania Bara na Visiwani, lakini bado tumejawa na amani kiasi kwamba unapokuwa kwenye ardhi ya Tanzania huna sababu ya kuwa na wasiwasi wowote kwa sababu wananchi wake wanaishi kwa upendo,” alisema Balozi Mgaza.
Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, maonyesho hayo kwenye ofisi yao waliyapa jina la Visit Tanzania the land Kilimanjaro, Serengeti and Zanzibar, ambapo pia walitangaza bidhaa za chai, kahawa, viatu vya kimasai, vinyago vya wanyama na nguo za utamaduni. (P.T)

Buhari aamuru uchunguzi tuhuma za ubakaji

No comments:



media
Rais wa Nogeria, Muhammadu Buhari asema kusononeshwa na ripoti ya Humana right Watch kuhusu tuhuma za ubakaji zinazowakabili askari wake.
Rais wa Nigeria ameamuru uchunguzi kuhusu madai ya unyanyasaji wa kijinsia katika makambi yaliyojengwa kwa minajili ya kuwapokea watu waliokimbia machafuko yaliyokuwa yakitekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram.
Kwa mujibu wa Ofisi ya rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari "alishtushwa" na ripoti ya shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) ambalo linawashtumu maafisa wa vikosi vya usalama vya nchi yake kuwabaka wanawake katika makambi hayo ya wakimbizi.
Rais Muhammadu Buhari ameitaka polisi na Wakuu wa majimbo husika kuanza mara moja uchunguzi ili kutoa mwanga juu ya madai ya HRW.
Kwa mujibu wa Human Right Watch, wanawake 43 walibakwa au kutumiwa kingono na maafisa wa usalama na makundi ya wanamgambo.
Vitendo hivi vya ubakaji vilifanyika katika makambi yaliyojengwa hasa katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi, kwa minajili ya kuwapokea watu waliolazimika kukimbia mauaji yaliyokua yakitekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram.
Baadhi ya wanawake waliokuwa wakiishi katika makambi wamesema walilazimishwa kufanya ngono na kutelekezwa wakati walipata ujauzito, kwa mujibu wa Human Rights Watch.
Machafuko yanayoendeshwa na kundi la kijihadi nchini Nigeria yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na watu zaidi ya milioni mbili wamelazimika kuyahama makazi yao.RFI

POLISI YAWASHIKILIA 200 KWA MAKOSA MBALIMBALI

No comments:



01
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu ya operesheni walizozifanya hivi karibuni leo jijini Dar es Salaam.
02
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha bunduki ambayo iliangushwa na wtu wanaodhaniwa kuwa majambazi leo jijini Dar es Salaam.
03
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha kwa waandishi habari  begi la bangi ambalo lilikuwa likiinga Dar es Salaam.
04
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha panga ambazo wamezikamata katika operesheni leo jijini Dar es Salaam.
05 06
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha gari la Polisi likiwa linabeba mzigo wa bangi uliokatwa na Polisi katika msako ulifanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu zaidi ya 200 kwa tuhuma mbalimbali likiwemo kwa watu Raia wa China kutapeliwa dola za kimarekani 800 kwa kutumia jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza na waandishi wa habari , Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amesema kukamatwa kwa watu hao imetokana na operesheni zinazoendelea katika jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wananchi na mali zao wanaishi kwa amani.
Amesema katika waliokamatwa ni pamoja ni panya road saba waliomvamia  Nyumbani kwa  Askari wa Jeshi la Wananchi , Ladislaus Kaitaba.
Katika tukio waliweza kukamata mtandao wa panya road kwa kutumia Ramadhani Ndabi (35)ambaye alichukua simu ya askari hiyo baada ya kupiga akapatikana na kuanza kutaja wenzie wanaofanya matukio.
Aidha amesema kuwa wizi wa magari unaendelea lakini polisi waliweza kukamata gari lilokuwa likiuzwa kwa kujifanya wateja na ilipogundulika walioiba wakatoweka.
Kamanda Sirro amesema kuwa bangi imekuwa ikiingzwa kwa njia nyingi na sasa watu wanatumia mabegi wakiwa wasafiri kumbe wanakuwa wameweka bangi. (P.T)

Dk. Shein akutana na ujumbe wa JICA

No comments:


ksi1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikianoya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki alipofika Ikulu Mjini Unguj,[ na Ikulu.]31/10/2016.
ksi2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikianoya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki (wa pili kulia) alipofika na ujumbe aliofuatana nao Ikulu Mjini Unguja,[ na Ikulu.]31/10/2016.
ksi3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikianoya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki alipofika Ikulu Mjini Unguja,[ na Ikulu.]31/10/2016. (P.T)

Kampuni ya Bayport yasherehekea miaka 10 ya kuanzishwa kwake pamoja na watoto wa KCVC

No comments:




Mgeni rasmi, Mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa, akiongea na wafanyakazi wa Bayport, waandishi wa habari na walimu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wakati wakusherehekea miaka 10 ya Bayport ambayo ilifanyika katika kituo hicho juzi, Kibaha mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport, John Mbaga, akiongea na wafanyakaziwa Bayport, waandishi wa habari na walimuwakituo cha kuleleawatotoyatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wakati wakusherehekeamiaka 10 ya Bayport ambayoilifanyikakatikakituohichojuzi, KibahamkoaniPwani.

Baadhi ya wafanyakazi wa Bayport Tanzania wakiwa valisha fulana watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Kibaha Children Village Center, wakati wafanyakazi hao walipokwenda kusherehekea miaka 10 ya kampuni hiyo

Wafanyakazi wa Bayport wakipiga picha ya pamoja kwenye bango lao

Watoto wakibembea wakati wa kusherehekea miaka 10 ya Bayport Tanzania

Watoto wakiwa wanakula pamoja kusherehekea miaka 10 ya Bayport Tanzania








Wafanyakazi wa bayport wakiwa katika picha ya pamoja naviongozi, watoto yatimanawatotowawafanyakaziwa Bayport Tanzania, wakati wa kusherehekea miaka 10 ya Bayport ambayo ilifanyika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wengine pichani (Kuliakwa Mama Mkapa) ni MkurugenziMtendajiwa Bayport John Mbaga na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano NgulaCheyo.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE

No comments:


 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger