
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte
Rais wa
Ufilipino Rodrigo Duterte, ameahidi kuacha kutumia lugha ya matusi baada
ya kile anachosema kuwa ni kupata ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa
Mungu.
Rais
huyo, alliyemwita Rais Barack Obama "mwana wa kahaba" na akasema
kiongozi huyo anaweza "kwenda jehanamu", amesema amefikia uamuzi huo
baada ya kupata ufunuo alipokuwa safarini kutoka Japan.
Amewatusi
pia watu wengine mashuhuri. Alimwita kiongozi wa kanisa Katoliki
duniani Papa Francis "mwana wa kahaba" (Ufilipino ni taifa lenye
Wakatoliki wengi).
Duterte
asema Obama anaweza 'kwenda jehanamu'Mfahamu rais Duterte, kiongozi
aliyemtusi ObamaRais wa Ufilipino atishia kuondoka UN
Amewahi
kumtusi pia waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kwa kumuita
"mwendawazimu" na majuzi alimweleza balozi wa Marekani nchini Ufilipino
kama "mpenzi wa jinsia moja ambaye ni mwana wa kahaba".
Bw
Duterte amesema kuwa alipokuwa kwenye ndege, na watu wengine wote
walikuwa wamelala, alisikia sauti ikimuonya: usipokoma, nitaiangusha
ndege hii.
Amesema sauti hiyo ilijitambulisha kuwa ilitoka kwa Mungu.
Amewaahidi watu waliokusanyika mji wake wa nyumbani wa Davao kwamba ahadi kwa Mungu ni sawa na ahadi kwa Wafilipino.
Rais Duterte ni kiongozi ambaye msimamo wake na matamshi yake huzua utata mara kwa mara.
Amesomea
taaluma ya sheria na alipanda cheo hadi kuwa mwendesha mashtaka kabla ya
kuteuliwa kuwa naibu meya wa Davao wakati wa mapinduzi yaliyomuondoa
madarakani Ferdinand Marcos mwaka 1986.
Alikuwa
meya mwaka 1988 na kushikilia wadhfa huo kwa kipindi cha miaka 10, kabla
ya kushinda kiti cha ubunge katika Bunge la Congress halafu akarejea
kwenye kiti cha umeya mwaka 2001.
Alijijengea
umaarufu kwa kupiga vita baadhi ya matatizo makubwa yanayowakabili
Wafilipino - uhalifu, makundi ya uasi, na ufisadi. Yote haya yalipungua
kwa kiwango kikubwa wakati alipokuwa kiongozi wa Davao, na kufanya mji
huo kuwa mmoja wa miji salama zaidi nchini Ufilipino.

Bw Duterte amesema anataka kuokoa Ufilipino kwa ajili ya vizazi vijavyo
Duterte
ambaye utawala wake ni wa kipekee kwa kuwa kiongozi mwenye sera za
Kijamaa na mwanamageuzi kwa pamoja, sera zake za uchumi zilikuwa si za
kuaminika wakati wa kapeni.
Majuzi, alilinganisha vita vyake dhidi ya walanguzi wa mihadarati na mauaji ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Alisema anaweza kuua walanguzi wengi wa dawa hizo za kulevya sawa na alivyofanya Hitler akiua Wayahudi.
"Hitler aliua Wayahudi milioni tatu ... kuna waraibu milioni tatu wa dawa za kulevya. Ninaweza kufurahia sana kuwaua," amesema.
Wayahudi zaidi ya milioni sita waliuawa na Wanazi chini ya Hitler.BBC
SHARE








No comments:
Post a Comment