TRA

TRA

Tuesday, February 28, 2017

President Obama and Michelle

No comments:




 Former US President Barack Obama and former first lady Michelle Obama intend to write separate books but want to sell the publishing rights in a package deal. FILE PHOTO


NEW YORK
Barack and Michelle Obama have signed a deal to publish their memoirs with New York-based Penguin Random House, in a coveted contract reportedly worth tens of millions of dollars.
America's first African American president is already the author of two memoirs and a children's book.
He has frequently declared himself to have a "writer's sensibility" and has said he does not want to write a conventional blow-by-blow account of his time in the White House.
Michelle Obama's memoir is likely to be just as eagerly anticipated.
A descendant of slaves, she became the first African American first lady and garnered high approval ratings - to the point where she was arguably one of the country's most respected and popular women.
Penguin Random House said in a statement it has "acquired world publication rights for two books, to be written by president and Mrs Obama respectively."
RECORD SUM
The terms of the deal were not disclosed, but bidding for the high-profile double book deal topped $60 million, a record sum for US presidential memoirs, according to the Financial Times.
Until now, the record for a US presidential memoir was $15 million paid for Bill Clinton's "My Life," released in 2004. George W. Bush received $10 million for "Decision Points" in 2010.
Hillary Clinton reportedly received a $14 million advance for "Hard Choices," her account of her time as secretary of state under Obama.
The Obama deal was negotiated by Washington super-lawyer Robert Barnett, who represented both the Clintons and Bush.
As part of the agreement, the company will donate one million books in the Obama family's name to First Book, a charity, Penguin said.
"We are very much looking forward to working together with President and Mrs Obama to make each of their books global publishing events of unprecedented scope and significance," said Penguin Random House CEO Markus Dohle.
The Obamas took a long vacation after Donald Trump was sworn in as president on January 20, and the former president has stuck by a pledge to keep a low public profile unless events threatening what he called America's "core values" warranted that he speak out.
He did just that in January, just days after Trump enacted his ban on travellers from seven mostly Muslim countries, and on all refugees. Obama expressed support for protests that sprang up nationwide against the now-suspended Trump travel ban.
Whereas US presidents tend to leave town after leaving the White House, the Obamas are settling into a rented mansion in Washington's posh Kalorama district until their younger daughter Sasha finishes high school. Their eldest daughter Malia will be attending Harvard in the fall.
Another new neighbour in Kalorama is Trump's daughter Ivanka, who has rented a house along with her husband Jared Kushner and their three children, near the Obamas.

Rais wa Somalia atangaza ''janga la kitaifa''

No comments:
Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo leo ametangaza ''janga la kitaifa'' kutokana na ukame mkali ambao mashirika ya misaada yamesema umewaingiza kiasi ya watu milioni tatu katika mzozo. Rais Farmajo ameiomba jumuiya ya kimataifa kushughulikia haraka mzozo huo ili kuzisaidia familia na watu binafsi kutoka katika janga la ukame na kuepusha maafa ya kibinaadamu. Shirika la Afya Duniani, WHO jana lilionya kuwa Somalia iko katika hatari ya kukumbwa na njaa kwa mara ya tatu ndani ya kipindi cha miaka 25. Njaa ya mwaka 2011 iliwaua kiasi ya watu 260,000. Wakati huo huo, ukame umesababisha kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile kuhara, kipindupindu na surua na karibu ya watu milioni 5.5 wako katika hatari ya kupatwa na magonjwa hayo.

Duterte aiomba radhi Ujerumani

No comments:
Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, ameiomba radhi Ujerumani kwa kushindwa kuzuia kuchinjwa kwa mateka wa Kijerumani aliyekuwa anashikiliwa na wanamgambo. Amesema operesheni kabambe ya ndege za kivita dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali inaendelea. Maafisa wa Ufilipino wamesema Jurgen Gustav Kantner aliuawa kwa kuchinjwa na wanagambo wa Abu Sayyaf kusini mwa Ufilipino baada ya muda uliowekwa kwa ajili ya kulipa fedha ili aweze kuachiwa huru kumalizika Jumapili. Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amelaani vikali mauaji hayo akisema hicho ni kitendo cha kuchukiza. Duterte ameelezea jinsi serikali yake inavyoshughulikia wimbi la utekaji nyara unaofanywa na wanamgambo hao wenye itikadi kali za Kiislamu, ikiwemo ombi kwa China la kusaidia katika doria katika eneo la bahari ya kimataifa linalopakana na kusini mwa Ufilipino, Malaysia na Indonesia, ambako matukio ya uharamia na utekaji nyara yamekuwa yakifanyika.

Trump kuliomba bunge liongeze bajeti ya ulinzi

No comments:
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema anataka kufanya ongezeko kubwa katika bajeti ya ulinzi. Ikulu ya Marekani imesema Trump anataka kuongeza matumizi katika jeshi la nchi hiyo kwa kiasi cha Dola bilioni 54. Trump amesema moja ya majukumu muhimu zaidi kwa serikali ya shirikisho ni bajeti ya Marekani. Afisa wa bajeti wa Ikulu ya Marekani, amesema Trump ambaye leo atalihutubia Bunge la Marekani kwa mara ya kwanza, ataliomba bunge hilo kuongeza matumizi ya Wizara ya Ulinzi katika mwaka ujao wa fedha kwa Dola bilioni 54, katika pendekezo lake la kwanza la bajeti na kupunguza kiasi kama hicho kutoka kwenye matumizi yasiyo ya ulinzi, ikiwemo kupunguza kwa kiasi kikubwa misaada kwa mataifa ya kigeni. Hata hivyo, wabunge wa chama cha Democratic na Republican ambao lazima waipitishe bajeti hiyo, wote wanalipinga pendekezo hilo.

Tuzo ya Mo Ibrahim 2016 yakosa mshindi

No comments:

Wakfu wa Mo Ibrahim umetangaza kwamba hakutokuweko na mshindi wa tunzo yake uongozi bora barani Afrika kwa mwaka 2016.
Tangazo hilo lilitolewa Jumanne ( Februari 28 )  kutokana na mkutano  wa kamati  uhuru  ya tuzo hiyo, chini ya Uweyekiti wa Dr Salim Ahmed Salim pamoja na  mkutano wa  bodi ya  wakfu huo uliofanyika  mwishoni mwa juma lililopita.
Akizungumzia juu ya uamuzi wa kamati  ya tuzo hiyo ya Mo Ibrahim, Dr Salim alisema " kama  ninavyosisitiza kila mwaka , paliwekwa kipimo cha hali ya juu, wakati tukizindua tuzo hii  2006.
Tunatambua na  kupongeza mchango muhimu unaotolewa na viongozi wengi wakiafrika kuleta mabadiliko katika nchi zao . Lakini tuzo hii inakusudiwa kumulika na kusherehekea uongozi  wa aina yake, jambo ambalo si la kawaida  ukizingatia kielelezo halisi."
Dr Salim akaongeza kusema kwamba baada ya zingatio makini, kamati hiyo imeamua  kutomzawadia yeyote tuzo hiyo kwa  mwaka 2016.
Libyen Sudan Dafur Freidensgespräche in Sirte (AP) Mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya Mo Ibrahim, Dk. Salim Ahmed Salim (kushoto) amesema kwa mara nyingine hakujapatikana mshindi wa tuzo hiyo.
Wagombea wote wa  tuzo ya Ibrahim ni ama Viongozi  wa taifa  au Serikali waliondoka madarakani katika kipindi cha miaka mitatu iliopita  na ambao walikuwa wamechaguliwa kidemokrasi na kutumikia vipindi vyao kwa mujibu wa katiba.
Tangu ilipoanzishwa 2006, tuzo ya Mo Ibrahim imeshatolewa mara nne. Washindi waliopita  ambao wote walikuwa marais wa nchi zao ni, Hifikepunye Pohamba wa Namibia (2014), Pedro Pires wa visiwa vya Cape Verde (2011), Festus Mogae wa Botswana  (2008) na Joaquim Chissano wa Msumbiji (2008). Rais wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela alitunukiwa  tuzo ya heshima  2007.
Wakfu wa Mo Ibrahim unatarajia kuwa na  tamasha maalum , " Wikiendi ya Utawala," mjini Marrakech Morocco kuanzia  Aprili7-9 2017. Tamasha hilo litafunguliwa Ijumaa jioni kwa mjadala wa ngazi ya juu uliopewa jina, " Mazungumzo kuhusu  Uongozi ", yakizingatia changamoto za  uongozi duniani katika karne ya 21 .

DC HAPI ATOA SIKU SABA KWA WACHIMBAJI WA KOKOTO KATIKA ENEO LA BOKO KUPISHA UJENZI WA DAMPO LA KISASA.

No comments:



Na Anthony John Glob ya Jamii.
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Alli  Hapi ametoa muda wa siku saba kwa wachimba kokoto wa eneo la Boko chama kuondosha mawe yao yaliyopo kwenye eneo hilo, ili kupisha ujenzi wa dampo la kisasa.

Kauli hiyo ya DC Hapi imekuja baada ya kutembelea na kukagua eneo hilo ambalo awali wachimbaji wake walipewa amri ya kutokuendelea na uchimbaji wa kokoto, lakini baadhi wamekaidi amri hiyo na kuendelea.

Akielezea zaidi Hapi amewataka kutokuendelea kuchimba na hasa katika kipindi hiki cha mvua, kwani wanaweza kujisababishia madhara ya kufukiwa na kifusi na kupoteza uhai.

Amesema amewaelekeza maafisa mazingira na mipango miji wa manispaa waunde timu ,waangalie uwezekano wa kuweka dampo kwenye eneo hilo, kwani eneo la dampo lililopo ni moja Pugu Kinyamwezi, ambako ni mbali.

Aidha amesema dampo hilo lifanywe la kisasa ili uwe mradi ambao utasaidia kuingiza mapato kwa manispaa.

Aidha HAPI ameeleza kuwa pindi eneo hilo litakapoanza kutengenezwa watu waliokuwa wakichimba hapo waandae orodha ya majina ili mawe yatakayotolewa hapo wapewe wao.

Kwa upande wake afisa mazingira wilaya ya kinondoni Mohamed Msangi amesema, eneo hilo likifanywa dampo litarahisisha utupaji taka kwa wakazi wa eneo la boko, mabwepande, bunju,  kawe na mwenge.
 Eneo linalochimbwa kokoto na baadhi ya Wakazi wa Boko chama,ambalo kwa sasa utaratibu wake umesitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh.Ally Hapi
 Mkuu wa wilaya  ya Kinondoni Ally Hapi akiwa na wakazi wa Boko chama katika eneo la uchimbaji wa kokoto
  Mkuu wa wilaya  ya Kinondoni  Ally Hapi  akizungumza  na watendaji wa Kata pamoja na wenyeviti wa Serikali za Mitaa jana katika Ofisi ya Afisa mtendaji wa Kata ya Bunju katika ziara yake ya siku kumi.
 Wenyeviti wa Serikali za mitaa na watendaji katika Kata ya bunju  wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kinondoni  Ally Hapi jana katika ziara yake.

ALLY KIBA APOKEWA KISHUJAA, AISIMAMISHA JIJI LA DAR ES SALAAM NA VIUNGA VYAKE

No comments:


 Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika
Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika

               

 Mashabiki wa AlyKiba ambao walifika katika uwanja wa ndege wa JNA jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango kama wanavyoenekana pichani
 Kiba kielekea kwenye gari maalum aliyoandaliwa mara baada ya kuzngumza na mashabiki wake
 Aly Kiba akiwa na Meneja wake  Seven Mosha mara baa da ya kuingia katika gari hiyo maaalum
 Ally Kiba akiwa katika mitaa ya Kariakoo huku akiwa amezunguskwa na mashabiki mbalimbali ambao walipata fursa ya kuona Tunzo yake ya Mtv base kama msanii bora wa kiume Afrika
 Mashabikiw a Ally Kiba wakiwa wamezunguka gari ya msanii huyo katika mitaa ya Kariakoo
 Ally kiba akiwa katika mtaa wa Mueza eneo alikokokulia akiwa na Tunzo yake

 Ally Kiba akiwa na Ndugu Yake Abdul Kiba juu ya gari la wazi katika mita aya Buguruni
 Ally Kiba akimkabidhi Tunzo yake Mama yake mzazi maarufu kama Mama k
 Mama K ambaye ni mama mzazi wa Ally Kiba akionyesha Tunzo ya msani huyo juu
Baadhi ya Mashabikiwa Ally Kiba wakiwa katika Pikipiki na shangwe ya Alli ya juu

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MARCH 1,2017

No comments:


 

MEYA JIJI LA TANGA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI AWATAKA KUCHAPA KAZI

No comments:


Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi akisisitiza jambo kwenye kikao cha baraza la madiwani leo kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni
Naibu Meya wa Jiji la Tanga,Mohamed Haniu akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani 
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji 
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizunguza kwenye kikao cha baraza la Madiwani leo kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni 
Baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga nao wakiwa makini kuchukua baadhi ya hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na madiwani kwenye kikao hicho cha baraza la madiwani 
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim akifuatilia kwa umakini kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Halmashauri Jijini Tanga. 
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia kwa umakini kikao hicho kulia ni Diwani wa Kata ya Central Jijini Tanga,Khalid Mohamed wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga wa kwanza kulia ni Mratibu wa Ukimwi Jiji la Tanga,Moses Kisibo anayefuatia ni Meneja Mkuu wa kituo cha Television ya Jiji la Tanga (TATV) Mussa Labani wakifuatilia kwa umakini majadiliano ya kikao hicho
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea mara baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Madiwani.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CCM).Alhaji Mustapha Selebosi kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji nyuma yao ni Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu mara baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Madiwani leo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger