TRA

TRA

Friday, May 19, 2017

MREMBO SHAMSA FORD ATOA FUNGO KWA MASTAA WA KIKE

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Shamsa Ford amefunguka kwa kuwaonya Mastaa wa Wanawake waache tabia za kuchagua wanaume wa kuwaoa, kwani leo wana majina makubwa na wanaonekana warembo lakini ipo siku itafika hata hao wanaume wanaowatongoza leo watapotea kabisa.

Shamsa Ford amesema kwa sasa Wanawake wenye majina makubwa wanajiona warembo kiasi kwamba hufikia hatua hata ya kusubiri wanaume matajiri wa kuwaoa bila kukumbuka kuwa hata hao matajiri wana watu wao huku wakisahau kuwa ndoa ni baraka toka kwa Mungu na ina heshima kubwa sana.
Wasichana wenzangu maisha ni mafupi sana leo tunavuma na kupendwa kila kona tunapokatiza ila kuna muda utafika hata nzi hakusogelei.Hata uwe mzuri na maarufu kiasi gani lakini ndoa ina heshima yake.Msiwe wachaguzi sana.Maana ukisema unamsubili tajiri aje akuoe na yeye huyo tajiri ana mwanamke wake aliyetoka naye mbali kimaisha.“Ameandika Mrembo Shamsa Ford kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiwapa somo wanawake wenzie kuhusu Mwanaume wa kuoa
Cha muhimu ni kumuomba Mungu akupe mwanaume mwenye kumjua Mungu,mwenye upendo,heshima,mtafutaji hayo mengine yanakuja tu..Nguvu ya mmoja ni tofauti na ya wawili “Ameandika Shamsa Ford.
Shamsa Ford kwa sasa yupo kwenye ndoa na mfanyabiashara Chidi Mapenzi

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger