RAPA
anayekuja kwa kasi Bongo, Harmorapa amefanya intavyuu na Mtangazaji wa
Kipindi cha Ala za Roho cha Couds FM, Diva The Bause, ambapo rapa huyo
amefunguka mambo kibao ikiwemo ishu ya kudai kuwa anampenda Malkia wa
Bongo Movies, Wema Sepetu.
Miongoni
mwa mambo aliyoyafungukia, Harmorapa ameeleza ukweli kuhusu ishu
iliyovuma miezi michache iliyopita, pale alipojinadi kwamba anampenda
sana Wema Sepetu na yupo tayari kufunga naye ndoa, ambapo Wema
alicharuka na kumjia juu.
Wema Sepetu
Ameeleza
ukweli wa ishu nzima na kama amewahi kuwa kwenye penzi la Wema au Laa.
Pia amesema siyo kweli kwamba yeye anapenda kiki bali kiki ndiyo huwa
zinamfuata. Akitolea mfano ishu ya kutolewa bastola kwa Nape Nnauye,
Harmorapa amesema kwamba alikuwa kwenye harakati zake akielekea kwenye
intavyuu kwenye redio moja Bongo ambapo alipofika Namanga ndipo
alipokutana na sakata hilo lililosababisha atoke nduki kali.
Kuhusu ishu ya yeye kudaiwa kutoka na Amber Lulu kimapenzi ambapo kwa sasa wameshaachana kutokana na kutofautiana naye.
Pia
ameeleza tofauti iliyopo kati yake na Harmonize japo wanatoka mkoa
mmoja wa Mtwara huku akianika mkali wa Bongo Fleva anayemkubalia na yuko
tayari kufanya naye kolabo kati ya Diamond na Ali Kiba.
SHARE









No comments:
Post a Comment