TRA

TRA

Friday, June 30, 2017

HANS POPPE: KWELI NIMEHOJIWA NA TAKUKURU

No comments:



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema alihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Hans Poppe amesema alihojiwa lakini akaachiwa na si anashikiliwa kama ambavyo imekuwa ikielezwa.

“Nilikwenda, nikahojiwa na baadaye nimeondoka, niko mitaani. Si kweli kwamba ninashikiliwa.

“Kuhusiana na kuhojiwa tayari nilihojiwa kama mara mbili hivi kabla. Haya ni mambo yanatokea,” alisema Hans Poppe.

Jana kulikuwa na taarifa kwamba Hans Poppe naye alikuwa anashikiliwa na Takukuru baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kupandishwa kizimbani.

Ama kweli raha ujipe mwenyewe. Daah ebu mtazame Obama hapa

No comments:


Serikali Yatoa siku 7 walimu Wapewe Posho Zao

No comments:




Serikali imetoa siku saba kwa ajili ya halmashauri zote kuhakikisha walimu wa hesabu, sayansi na wataalamu wa maabara waliopangwa hivi karibuni wanapewa posho za kujikimu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (Chadema).

Mkundi alitaka kujua ni lini serikali itawalipa stahiki zao walimu wa Hesabu, Sayansi na watalaamu wa maabara waliopangiwa vituo hivi karibuni.

Alisema halmashauri zote zilizopokea walimu hao zinapaswa kuwapa posho za kujikimu ndani ya siku saba.

Akijibu swali la msingi la Mkundi aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa posho za mazingira magumu kwa watumishi wa maeneo ya pembezoni, alisema, “Katika kutekeleza Sera ya Malipo ya Mishahara na Motisha iliyopitishwa mwaka 2010, mwaka 2012/13 halmashauri 33 za wilaya ikiwemo halmashauri ya Ukerewe ziliwezeshwa kuandaa miongozo ya kutoa motosha kwa watumishi.”

Alisema kutokana na mpango huo, halmashauri 29 ziliandaa na kuwasilisha katika ofisi ya wizara hiyo miongozo iliyobainisha aina ya motisha inayohitajika.

“Utekelezaji wa miongozo hiyo kwa halmashauri zote 29 ulikadiriwa kugharimu Sh bilioni 331.087 kwa mwaka na utekelezaji wa miongozo hiyo, ulitarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha wa 2013/14 na haukuanza kutokana na ufinyu wa bajeti."

Ndege ya Rais wa Nigeria yaegeshwa kwa siku 50 London

No comments:
Ofisi ya Rais nchini Nigeria imekiri kuwa ndege rasmi ya Rais Muhammadu Buhari imeegeshwa kwa zaidi ya siku 50 kwenye uwanja wa ndege mjini London.

Rais Buhari ambaye ni mgonjwa aliondoka nchini Nigeria kwa likizo ya kimatibabu tarehe 7 mwezi Mei akiitumia ndege hiyo.

 Rais Muhammadu Buhari (kushoto) na makamu wake Yemi Osinbajo

Ofisi ya Rais ilikuwa ikijibu ripoti za mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu nchini Nigeria, wameelezea ghadhabu yao kutokana na kuegeshea ndegr hiyo mjini London.
Ilidaiwa kuwa ndege hiyo inalipigwa pauni 4000 kwa siku kama ada ya kuiegesha, katika uwanja wa Stansted mjini London, na kwa muda wa siku 50 imegharimu nchi hiyo pauni 200,000.

Msemaji wa Rais, Garba Shehu, alikana kuwa nchi inalipa pesa nyingi kwa nafasi hiyo. Aliiambia BBC kuwa gharama ya kuegesha ndege hiyo haitazidi pauni 1000.

Rais  Buhari amekuwa nje ya nchi kwa karibu miezi miwili kupata matibabu mjini London.

Ujerumani yaichapa Mexico 4-1 kombe la mabara

No comments:

Iliwachukua Mexico dakika 89 kuweza kumfunga Marc-Andre ter Stegen

 

Ujerumani imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mabara baada ya kuichapa bila huruma Mexico 4-1.

Leon Goretzka alifunga mara mbili katika mtanange huo katika dakika ya 6 na 8.

Magoli mengine ya Ujerumani yaliwekwa kimiani na Timo Werner dakika ya 59 na Amin Younes dakika ya 90.






Goli la kufutia machozi kwa upande wa Mexico lilipachikwa na Marco Fabian dakika ya 89.

Mexico walipata nafasi nyingi lakini hawakuweza kuzitumia vyema huku Ujerumani ikionekana kukomaa vilivyo katika safu ya ulinzi.

Fainali ya kombe la mabara itapigwa jumapili ya Julai 2 mbili kati ya Ujerumani na Chile mjini St Petersburg, huku mchezo wa awali ukizikutanisha Ureno na Mexico kutafuta mshindi wa tatu.

Venus Wiliams ahusika katika ajali mbaya ya barabarani

No comments:


 
Nyota wa mchezo wa tenisi Venus Williams amehusika katika ajali mbaya ya barabarani iliomuua mwanamume wa miaka 78.

Msemaji wa kituo cha polisi cha Palm Beach Gardens mjini Florida aliithibitishia BBC kwamba walikuwa wanachunguza ajali hiyo iliomuhusisha bingwa huyo wa taji la Grand Slam.

"Mtu mmoja alipelekwa hospitali baada ya ajali hiyo iliofanyika tarehe 9 mwezi Juni na kufariki wiki mbili baadaye kutokana na majeraha ," alisema.

Kulingana na chombo cha habari cha TMZ, ambacho kilitoa habari hiyo, maafisa wa polisi wanaamini kwamba Williams ni wa kulaumiwa lakini wakili wake anasema kuwa ilikuwa ajali.

Nyota wa mchezo wa tenisi Venus Williams amehusika katika ajali mbaya ya barabarani iliomuua mwanamume wa miaka 78.

Mtu aliyefariki ,Jerome Barson, alikuwa akisafiri na mkewe aliyekuwa akiendesha gari hilo kupitia eneo la makutano wakati ajali hiyo ilipotokea.

''Gari la bi Williams lilingia kwa haraka katika barabara yao halikuweza kuondoka kwa haraka kutokana na msongamano wa magari barabarani kulingana na taarifa ya shahidi katika ripoti ya polisi iliopatikana na vyonbo vya habari.

Bi Barson pia alipelekwa hospitalini lakini akapona.
Bi Williams ana makosa kwa kukiuka sheria ya kumpatia heshima dereva aliye na haki ya kupita, ripoti hiyo ilisema, ikiongezea kwamba hakukuwa na maswala mengine kama vile ushawishi wa dawa za kulevya, pombe ama hata kusumbuliwa na simu ya rununu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi kuhojiwa kwa matumizi ya nguvu

No comments:
 
 Antonio Benavides anasema ni vigumu kutumia njia ya   kawaida kuwakabili waandamanaji wasiochoka


Ofisi ya Mwanasheria Mkuu nchini Venezuela imemtaka mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi kutoa maelezo juu ya matumizi ya nguzu zilizopitiliza dhidi ya mamiz ya waandamanaji wanaoipinga serikali nchini humo.

Ofisi hiyo imesema kuwa kuna ushahidi wa kutosha juu ya matumizi ya nguvu zilizopitiliza kwa waandamanaji.
Antonio Benavides anatarajiwa kuhojiwa siku Julai sita. 

Aliondolewa madarakani wiki iliyopita, baada ya polisi aliowapa maelekezo kuonekana wakiwafyatulia risasi waandamanaji.
Zaidi ya watu 80 wameuawa katika maandamano ya miezi mitatu ya kupinga utawala wa Rais Nicolas Maduro.

CHANZO: BBC

Trump na Putin uso kwa uso wiki ijayo

No comments:
Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Rais Donald Trump atakutana na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin wiki ijayo, ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G20).

Itakuwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana baina ya viongozi hawa wawili.

 Trump na Putin walikubaliana kufanya kazi pamoja siku za nyuma 

Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani H.R. MacMaster amesema bado hakuna mada maalumu iliyopendekezwa.
Mapema msemaji wa ikulu ya Kremlin alithibitisha uwepo wa mkutano huo.

IGP SIRRO AWATIA MOYO WANAKIJIJI WA MICHUKWI, WILAYANI KIBITI

No comments:

3



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akikagua nyumba iliyochomwa moto na wahalifu waliofanya mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji cha Mangwi, kata ya Mchukwi wilayani Kibiti Juni 29, 2017 alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji  hayo.(PICHA NA HASSAN MNDEME WA JESHI LA POLISI)

unnamed
IGP Sirro akisalimiana na wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji.

1
Mkuu wa Meshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mangwi, kata ya Mchukwi wilayani Kibiti mkoani Pwani Juni 29, 2017 alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji hicho. IGP Sirro alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo na kuwataka kuwa na ushirikiano na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.


2
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa wananchi wa kijiji cha Mangwi, kata ya Mchukwi wilayani Kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na ofisa mtendaji wa kijiji hicho

PPF YATANGAZA MAJINA YA WATU WALIOCHAGULIWA KWA AJILI YA USAILI NAFASI ZA UDEREVA

No comments:


 

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA ,ASHUHUDIA MAGARI 103 YAKIWA NA SHEHENA YA MAHINDI NJIA PANDA YA HIMO

No comments:


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo Kamanda wa Polisi ,Hamis Issah na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba wakitembelea maeneo ambayo yameshikiliwa magari yaliyobeba shehena ya Mahindi .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizunbgumza na baadhi ya wafanyabaishara wa Mahindi ambao magari yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Wafanyabiashara ambao Mahindi yao yanashikiliwa katika eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipofika eneo hilo kwa lengo la kuzungumza nao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza na baadhi ya madereva na Wafanyabaisahara ambao Mahindi yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akitizama Malori yenye Shehena ya Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyuma ya vituo vya Mafuta .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akiongozana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issa wakiodoka katika eneo hilo baada ya kuangalia malori yanayoshikiliwa yakiwa na shehena ya Mahindi.
Baadhi ya Magari yakiwa yameegeshwa katika maeneo tofauti tofauti yakiwa na shehena ya Mahindi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.


ENEO la njia Panda linalounganisha barabara za Moshi/Arusha,Tanga/Dar es Salaam na ile ya Holili mpakani mwa nchi jirani ya Kenya linatajwa kama kituo kikuu cha malori yanayosafirisha nafaka kwenda nchi jirani ya Kenya.
Uchunguzi uliofanywa na Globu ya Jamii umebaini kuwepo kwa maeneo yasiyo rasmi ya kuegesha malori hayo ,mengine yakiwa na matela yake ,ambako shughuli za kupakua mahindi na kupakia katika magari madogo aina ya fuso zinazotoka nchi jirani ya Kenya hufanyika.
Maeneo mengine yanayotajwa kuwepo na Magulio  ya Mahindi ni katika sehemu za maegesho ya magari  zilizopo katika  vituo mbalimbali vya kuuza Mafuta ,pamoja na baadhi ya nyumba za wageni ambazo zimegeuzwa Maghala ya kuhifadhia Mahindi.
Magari zaidi ya 103 yanashikiiwa katika maeneo ya Njia Panda na Himo yakiwa yamebeba Shehena ya Mahindi tayari kusafirishwa huku baadhi ya madereva wakiyatelekeza Malori yao kwa siku ya tano sasa na kwenda kusiko julikana .
Hatua iliwasukuma Wafanyabiashara wa Mahindi pamoja na Madereva kufika ofisi za Mkuu wa mkoa kuwasilisha malalamiko yao juu ya kukamatwa kwa Malori hayo yakiwa Njia Panda badala ya mpakani kama alivyo agiza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.
Wakizungumza nje ya jingo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wafanyabiashara hao ,Laurance Kanyota,Nuru Madai na Mariam Ramadhan walisema wameshangazwa na hatua ya jeshi la Polisi kushikilia magari yao yalikuwa na Mahindi yakisafirishwa kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi.
“Magari yetu yapo pale Sheli Maount Meru,yalitokea Tunduma kwenda Arusha,yalipofika pale siku ya Jumamosi madereva walienda kula siku kuu ya Idd,jana (Juzi) asubuhi  Matandiboi wakapiga simu kwamba tumezungukwa na Polisi ,tukaenda pale tukaonana na OCD tukaliza kwanini mnatushikia magari ambayo yako Njia Panda yanayoenda Arusha au Moshi ,wakajibu tumetumwa kushika magari yote ya Mahindi.”alisema Mfanyabiashara Mariam.
Alisema alimuelewa Waziri Mkuu katika agizo lake kwamba magari yaliyopo mpakani ndio yashikiliwe  na si kama lilivyofanya jeshi la Polisi kukamata magari yaliyokuwa Njia Panda kuelekea Moshi na Arusha huku wakimuomba Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi  kwa wasaidizi wake juu ya agizo lake.
Mfanyabiashara Kanyota alisema amekuwa akifanya biashara ya kusafirisha mazao kwa njia halali ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi lakini anashangazwa na hatua ya kuzuiliwa kwa  Mahindi yake ambayo amekuwa akinunua na kuyauza katika viwanda vya kutengeneza unga kwa ajili ya Chakula.
“Tulikua tunaomba Mkuu wa mkoa ajue kwamba sisi ni wafanyabiashara tunaolipa kodi halali ya serikali atusaidie tufikishe mazao yetu sehemu yanapotakiwa kufika ,Mahindi yangu yanatoka Mbeya ,mkulima aiyeniletea mimi kama Dalali ametoka Tunduma.”alisema Kanyota.
Kauli ya Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro imepigiria msumari katika Agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kutaifisha Mahindi pamoja na gari litakalokutwa kuanzia June 26 mwka huu likiwa limebeba na kusafirisha Mahindi kwenda nje  ya nchi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Anna Mghwira  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa alisema jana ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari kuwa magari 103 yaliyokamatwa Himo na Njia Panda yatahesabiwa kama sehemu ya uhujumu uchumi na kwamba yatataifishwa .
“Magari yaliyokamatwa kule Siha ,tayari tulikwisha amua kwamba yatapelekwa Nationa Milling(Ghala la chakula la taifa)  Arusha ,lakini haya ya Himo ,Waziri Mkuu Alisha agiza kwamba kuanzia tarehe 26 ,magari yote yatakayokamatwa ,Bidhaa pamoja na magari yenyewe yatahesabiwa kuwa ni sehemu ya uhujumu Uchumi ,kwa hiyo yatataifishwa.”alisema Mghwira.
Mghwira alisema baada ya mfululizo wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro juu swala zima la uuzaji na usafirishaji wa chakula nje ya nchi,kamati imefanyia kazi tamko la Waziri Mkuu kutaka kujiridhisha vya kutosha juu ya hali ya chakula iliyopo Kilimanjaro na mikoa ya jirani.
“Uogozi wa mkoa wa Kilimanjaro unapenda kuwatangazia wananchi wote,hususani Wafanyabiashara wa Sukari na Nafaka za Mpunga,Mchele ,Mahindi na Unga wa Mahindi ya kuwa ni marufuku kwa mfanyabiashara yoyote au mwananchi yoyote kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi bila kibali cha serikali”alisema Mkuu huyo wa Mkoa .
Alisema kukiuka agizo hilo ni kuhujumu uchumi wa nchi  kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu cha 3 cha jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu Uchumi sura ya 200 ya sheria za Tanzania na pia ni kukiuka agizo la Waziri Mkuu,kupitia waraka wake alioutoa  Mei 30,2017,uliozuia utokaji  wa vyakula na sukari kwenda nchi jirani .
Alisema kwa kukiuka sheria hiyo kunaweza kusababisha upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini na kusababisha Mamlaka ya Mapato hapa nchini (TRA)  kukosa takwimu muhimu wa bidhaa zinazosafirishwa nje
“Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro imejiridhisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha sukari  na nafaka hizo nyakati za usiku na hiki ndicho kinaleteleza kukosa takwimu muhimu kwa kupitia njia ambazo si rasmi kwa kushirikiana na baadhi ya askari polisi ambao sio waaminifu.
Wakati wa baraza la Idd lilifanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi,Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa alitangaza kupiga marufuku usafirishaji wa Mahindi kwenda nchi jirani na kwamba atakaye kiuka utaratibu huo atahukuliwa hatua kali za kisheria.

Thursday, June 29, 2017

Nukuu muhimu kutoka kwa Martin Lurther King

No comments:
"Wenye hekima huongea kwa sababu wana kitu cha kuongea, lakini wapumbavu huongea kwa sababu wanataka kusema kitu"-Martin Lurther King


Airtel mwendo mdundo Maonesho ya Sabasaba, yatoa ofa kabambe

No comments:






Meneja Uuhusiano wa Airtel,  Jackson Mmbando  (kulia)  na Ofisa huduma kwa wateja wa Airtel,  Veronica Valentine (kushoto) wakionesha simu aina ya ZTE na Motorola katika banda la Airtel lililoko katika viwanja vya maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba, simu hizo zitauzwa kwa bei ya ofa ya shilingi 16,000 tu na mteja ataunganishwa na kufurushi cha muda wa maongezi kwa mwezi mzima cha shilingi 10,000 BURE. Katikati ni Ofisa huduma kwa wateja wa Airtel, Tumwidike Michael
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imetangaza ofa kabambe wakati wote wa maonyesho ya biashara ya sabasaba mwaka huu zitakazowawezesha wateja wake na wale  wapya kuunganishwa na huduma za mtandao kwa gharama nafuu na pia kujipatia simu bomba kwa bei nafuu.

Akiongea na waandishi wa habari katika banda la Airtel lililopo viwanja vya sabasaba Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “dhamira yetu Airtel ni kuendelea kuunganisha jamii kwa bidhaa na huduma, hivyo kwa msimu huu maonesho ya saba saba tutatoa ofa nyingi sana ikiwemo  simu aina ya ZTE GS 500, Motorola C113, Motorola F3 na Motorola C117 kwa sh. 16,000 tu na  mteja akishanunua ataunganishwa na bando la sh. 10,000 litakalodumu kwa muda wa mwezi mmoja”

“Unaweza ukaona hapo gharama ya simu inakuwa nafuu na kisha  unaunganishwa na kifurushi cha mwezi mzima BURE kuongea na ndugu, jamaa, na marafiki huku ukifaidi huduma zingine za Airtel” alieleza Mmbando

Katika banda letu ndani ya saba saba mwaka huu pia huduma zitakazopatikana ni pamoja na   kubadilisha laini, huduma za Airtel Money, simu za smartphone za kisasa na origino, huduma ya Timiza Vicoba, kuelekezwa jinsi yakusoma masomo ya ufundi kwa njia ya simu VETA kupitia Vsomo pamoja na kujua jinsi yakufungua biashara ya Duka la Airtel popote na jinsi ya kupata faida yako”

Mmbando alisema kuwa “Airtel imekuwa ni desturi yetu kuleta huduma na bidhaa zetu katika maonyesho haya ya biashara kila mwaka na kukutana na wateja wetu ana kwa ana ili kutoa elimu zaidi kuhusu huduma zetu mpya na za kibunifu tunazozitoa kila mwaka”.

“Natoa wito kwa Watanzania kutembelea banda letu na kujipatia simu huduma za kimtandao zote kwa  gharama nafuu na vilevile kukutana na watoa huduma wetu na kupata elimu juu ya huduma mbalimbali  ikiwemo Kupata maelekezo ya kupata mikopo ya vikundi kupitia huduma ya Timiza vikoba.    Kupata maelekezo ya kuweza kufanya biashara za Airtel kokote Tanzania kupitia mfumo wa Maduka ya Airtel AMSHA pamoja na huduma nyingine nyingi” aliongeza Mmbando.
 

Kwa raha zao. Hawa ni maofisa wa LAPF wakiwa Maonesho ya Tantrade. Waone ufurahie huduma zao

No comments:
 
4
Rehema Mkamba Ofisa Masoko Mwandamizi LAPF akisoma waraka wa Matangazo ya vipindi kutoka kampuni ya PPR iliyotembelea katika banda la mfuko huo lililopo kwenye Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TANTRADE barabara ya Kirwa kwa lengo la kutangaza huduma zake  katika maonyesho ya 41 ya baiashara ya nje  yanayoendelea jijini Dar es salaam.
1
Juma Milinga Ofisa Matekelezo Mwandamizi LAPF akimpa maelezo Bw. Nungu Weswa mteja aliyetembelea katika banda hilo ili kuionea huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo.
2
Kulia ni Simboninsia Ndosi Afisa Mafao LAPF na Sophia Matangalu Ofisa Mafao Mwandamizi LAPF wakiwa katika maonyesho hayo ili kutoa maelezo mbalimbali kwa wateja wanaotembelea kwenye banda hilo.
3
Ofisa Matekelezo LAPF,  Agness William akiwa tayari kwa kupokea wateja wanaotembelea katika banda hilo wakati huu wa maonyesho ya sabasaba kwenye viwanja vya TANTRADEBarabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
  5
Baadhi ya wafanyakazi wa mfuko huo wakitoa huduma kwa wateja mbalimbali waliotembelea katika banda la LAPF kwenye viwanja vya Maonyesho vya TANTRADE Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam, Kulia anayepata maelezo ni Cyprian Mpinda Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM.
6
Baadhi ya wafanyakazi wa LAPF wanaotoa huduma katika maonyesho hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
7
Muonekano wa banda la LAPF.

Kama kawaida yao, Azania Bank tayari wapo Sabasaba kushiriki Maonesho ya Tantrade

No comments:
 
az1
Mtaalam wa Mikopo ya Nyumba (Mortigage Specialist) kutoka Benki ya Azania, Liberia Peter akitoa maelezo kwa Allan Rukantabula kutoka kampuni ya Brighter Monday Tanzania aliyetembelea katika banda hilo kwenye maonyesho ya 41 ya TANTRADE yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kirwa jijini Dar es Salaam.
az2
Mtaalam wa Mikopo ya Nyumba (Mortigage Specialist) kutoka Benki ya Azania,  Liberia Peter na Allan Rukantabula kutoka kampuni ya Brighter Monday Tanzania wakifurahia jambo wakati mteja huyo  alipotembelea katika banda la benki hiyo kwenye maonyesho ya 41 ya TANTRADE yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
az3
Othman katikati , Victor kushoto na Liberia wafanyakazi wa Benki ya Azania wakiwa katika banda lao kwenye maonyesho ya 41 ya TANTRADE yanayoendelea kwenye viwanja vya maonyesho vya Sabasaba Baraara ya Kirwa jijini Dar es salaam.

Kumekucha Sabasaba. Unawafahamu PROPERTY INTERNATIONAL nenda uone huduma zao

No comments:


P1
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem akishauriana jambo na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Masoud Alawi katika banda la kampuni hiyo lililoko katika viwanja vya TANTRADE Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam ambapo maonyesho ya biashara ya Sabasaba yanaendelea kuanzia jana na yataendelea kwa muda wa siku kumi .
Kampuni hiyo inajishughulisha na upimaji wa viwanja na kuuza kupitia mabenki mbalimbali ambayo wameingia mkatataba nayo katika mpango huo  mabenki  yataweza kumlipia mteja wa kiwanja kwa mkopo alafu mteja atarejesha rejesho kidogokidogo mpaka atakapomaliza mkopo wake na kukabidhiwa hati ya kumiliki kiwanja chake muhimu mteja atatakiwa kulipa asilimia 5 mpaka 20 mwanzo wa mkopo wake kulingana na makubaliano ya kiwanja anachohitaji.
Kampuni hiyo pia inajishughulisha na ujenzi wa nyumba na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa visima vya maji, Katikati katika picha ni Bw. Suleiman Abdallah Mchoraji wa ramani za majengo  kutoka kampuni ya Property International.
P2
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Masoud Alawi akitoa maelezo kwa wateja waliotembelea katika banda hilo leo ili kujionea mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na bidhaa zinazopatikana katika banda hilo kulia ni Bw. Suleiman Abdallah Mchoraji wa ramani za majengo  kutoka kampuni ya Property International.
P03
Bw. Suleiman Abdallah Mchoraji wa ramani za majengo  kutoka kampuni ya Property International akitoa maelezo kwa Bw. Mahuna Tendwa kutoka Suma JKT aliyetembelea katika banda la Property International katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Masoud Alawi.
P3
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem akishirikiana na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kutoa maelezo na kuonyesha ramani za viwanja vilivyopo jijini Dar es salaam na mkoa wa Pwani kwa wateja mbalimbali waliotembelea banda hilo.
P4
Mmoja wa wafanyakazi akiwa katika banda hilo ili kutoa huduma kwa wateja wanaotembelea katika maonyesho hayo.
P5
Wateja wakiendelea kupata huduma katika banda hilo.
P6
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa na nyuso za bashasha wakati wakikaribisha wateja katika banda ka kampuni hiyo.
P7
Baadhi ya bidhaa zinazoonyeshwa katika banda hilo.
P8
Bw. Abdul Msalam Mtaalam wa masuala ya uchimbaji wa visima kutoka kampuni hiyo akiwa katika eneo lake kama zinavyoo pampu mbalimbali maalum kwa ajili ya visima virefu na vifupi.
P9
Muonekano wa Banda la Property International linavyoonekana.
 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger