
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga SC imeanza msimu kwa sare ya
kufungana goli 1-1 na Lipuli FC ya Iringa timu ambayo imepanda daraja
msimu huu ikiwa inafundishwa na kocha Selemani Matola mchezo uliopigwa
kwenye uwanja wa Uhuru ‘Shamba la Bibi’ jijini Dar es salaam.
Lipuli ilianza kupata dakika ya
44 baada ya Seif Abdallah kuachia shuti kali lililomshinda golikipa wa
Yanga Youthi Rostand kisha mpira kujaa wavuni baada ya kuwachachafifya
mabeki wa Yanga upande wa Gadier Mbaga.
Yanga walisawazisha bao dakika ya
45 goli ambalo limefungwa na Donald Ngoma aliyeunganisha kwa kichwa
mpira wa kona uliopigwa na Juma Abdul.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote kufanya mabadiliko hata hivyo mabadiliko hayakuweza kusaidia timu
zote kuweza kuondoka na pointi tatu na dakika za lala salama Lipuli
walipata pigo baada ya beki wao Kwansi Asante kuoneshwa kadi ya pili ya
njano na kuwa nyekundu.
SHARE








No comments:
Post a Comment