
Mabingwa
watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga SC imeanza
msimu kwa sare ya kufungana goli 1-1 na Lipuli FC ya Iringa timu ambayo
imepanda daraja msimu huu ikiwa inafundishwa na kocha Selemani Matola
mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru ‘Shamba la Bibi’ jijini Dar es
salaam.Lipuli
ilianza kupata dakika ya 44 baada ya Seif Abdallah kuachia shuti kali
lililomshinda golikipa wa Yanga Youthi Rostand kisha mpira kujaa wavuni
baada ya kuwachachafifya mabeki wa Yanga upande wa Gadier Mbaga.
Yanga
walisawazisha bao dakika ya 45 goli ambalo limefungwa na Donald Ngoma
aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Juma Abdul.
Kipindi
cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo mabadiliko
hayakuweza kusaidia timu zote kuweza kuondoka na pointi tatu na dakika
za lala salama Lipuli walipata pigo baada ya beki wao Kwansi Asante
kuoneshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu.
SHARE








No comments:
Post a Comment