Ndege
ya uzinduzi ya Shirika la Ndege la Etihad ikipokelewa na magari ya
zimamoto yaliyomwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege
kati ya jiji la Perth Australia na Abudhabi.
Ndege
ya Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad Boeing 787 Dreamliner imetua kwa
mara ya kwanza katika Jiji la Perth nchini Australia baada ya
kuzinduliwa kwa safari zake rasmi ikitokea Abu Dhabi.
Ndege
ya Etihad EY486 iliondoka Abu Dhabi siku ya tarehe 02 Juni muda wa saa
nne na nusu usiku na kuwasili Perth mji mkubwa uliopo magharibi mwa
Australia saa saba na nusu mchana ambapo ilipokelewa rasmi kwa tamaduni
za uzinduzi wa ndege mpya.
Ndege ya kurudi, EY487 iliondoka Perth saa 11 jioni na kuwasili Abu Dhabi saa sita na dakika 25 usiku wa tarehe 3 Juni.
Ndege
hiyo ya B787-9 Dreamliner ya Etihad ni bora na kisasa kwa abiria kwa
madaraja yote. Ina jumla ya viti 299 na ina uwezo zaidi ya asilimia 14
ukilinganisha na ndege ya Airbus A330-200. Kwa abiria wa daraja la juu,
ni zaidi ya asilimia 27 kwa ubora wa viti vyake.
Makamu
wa Rais wa Masoko wa Shirika la Ndege Etihad, Shane O’Hare alisema
uamuzi wa kuleta ndege bora zaidi unaendana na umuhimu kibiashara baina
ya Austaria Magharibi na shirika hilo.
“Tangu
tumezindua usafiri wa ndege kati ya Perth na Abu Dhabi miaka miwili
iliyopita, tumefurahia kuhudumia watu wa madaraja tofauti kwa
mafanikio.”
“Dreamliner
imeongeza nafasi 518 kwa wiki katika safari za anga, jambo hili
linatupa nafasi zaidi kuendana na mahitaji halisi ya wateja wetu.”
“Imewezesha pia wageni wetu kusafiri kwa raha mustarehe, huduma bora na ukarimu kutoka kwa wahudumu wetu wa Etihad.”
“Ndege
hiyo ya kisasa imeundwa kuendana na mahitaji mbalimbali ya weteja wetu,
ikiwamo sehemu kubwa ambayo watapata viburudisho, pia ikiwa ni ndege
bora zaidi kwa safari za mbali na karibu, huku huduma mbalimbali za
burudani zikiwemo ndani ya ndege pamoja na huduma za kiwango cha juu.”
“Bwana O’Hare aliongeza kuwa, “Kuanzishwa kwa huduma ya ndege ya Dreamliner kutawezesha kukuza utalii Magharibi mwa Australia.”
“Kwa
kuongeza safari za ndege kwa wiki Perth, Shirika letu la Etihad litakuwa
chachu ya kuongeza ukuaji katika sekta ya utalii ambapo itawezesha watu
mbalimbali kutoka ulimwenguni kote kutembelea hata wakati wa
mapumziko.”
“Kwa
pamoja na washirika wetu wa masuala ya usafiri, tunatoa huduma za
usafiri Ulaya, Mashariki ya Kati na ukanda wa kaskazini Marekani na hii
sasa inatoa huduma bora kati ya Perth na Abu Dhabi.”
Ndege
ya Etihad b787-9 iliyo katika kiwango cha juu ni matarajio itawahudumia
watu wengi hapo baadaye ikiwa na vyumba maalumu vilivyosheheni kila
huduma kwenye daraja la kwanza 28 na viti 271 kwenye daraja la kati.
Katika
daraja la kwanza kuna vyumba maalumu vyenye huduma zote muhimu vikiwa
na nafasi ya kutosha pamoja na huduma ya kitanda. Pia, daraja la kwanza
kuna mifumo mizuri ya ambayo itamwezesha abiria kusogeza kiti chake
kadiri anavyopenda huku akiburudika na runinga ya kisasa pamoja na vifaa
vya kuvaa masikioni vinavyomwezesha kupunguza kelele.
Aidha
daraja la kati lenye viti 271 inampa mteja nafasi ya kupumzika kupitia
kwenye kiti chake kwa namna kilivyotengenezwa ikiwa ni pamoja na kupata
ya huduma ya runinga yake binafsi kwenye kiti chake.
Abiria
akiwa kwenye Dreamliner atapata burudani ya muziki iliyounganishwa
kwenye ndege hiyo. Huduma hiyo inapatikana kwa masaa yote uwapo kwenye
ndege. Pia, kuna chaneli zinazorusha matangazo yake ya live huku zikiwa
ni screen ambazo zina kiwango cha ubora wa hali ya juu huku zikimfanya
abiria kujisikia vizuri.
Pia, hudma ya simu na wi-fe pamoja na sehemu za kuchomeka USB zinapatikana kwenye kila kiti.
Etihad
limekuwa shirika linaloongoza kwa huduma bora zinazotolewa ndani ya
ndege ikiwa na watoa huduma wenye uzoefu. Watoa huduma hao wana mafunzo
ya kutosha kutoka kwenye vyuo vinavyotambulika kimataifa ambao
watamsaidia abiria kila anapohitaji msaada hususani wale wanaosafiri na
watoto.
Vyakula
bora na salama vinavyopikwa na wataalamu kutoka hoteli maalumu,
vinatolewa kwenye daraja la kwanza na wengine wanaweza kupata huduma
hiyo kulingana na mahitaji ya abiria.
Shirika
la Etihad ndilo shirika pekee linalotoa huduma ya usafiri kutoka
magharibi mwa Australia na USA ikiunganisha na uwanja wa Ndege wa Abu
Dhabi. Ipo huduma inayomwezesha mgeni kukamilisha masuala ya uhamiaji na
ukaguzi wa kiusalama kwa USA wanaposafiri kwenda Abu Dhabi ili
kupunguza usumbufu wanapowasili uwanja wa ndege wa Marekani.
Shirika la Etihad lilizindua safari za Airbus A330-200 Perth Julai 2014.
Tofauti
na Perth, Shirika la Etihad pia linaunganisha zaidi ya miji 8 magharibi
mwa Australia. Etihad imefanikiwa kuunganisha watu na miji ya Broome,
Geraldton, Kalgoorlie-Boulder, Kununurra, Karratha, Paraburdoo, Port
Hedland na Newman.
Vilevile
Shirika la Etihad linatoa huduma katika mji wa Sydney ikiwa na safari
mara mbili kwa siku ikiunganisha na Virgin Australia, pia mara mbili kwa
siku Melbourne na mara mbili kwa siku mji wa Brisbane.
Perth
ndiyo mji wa pili kwa ukubwa Australia unaohudumiwa na ndege ya kisasa
ya Shirika la Etihad B787-9 Dreamliner na kwa mji wa Brisbane ilianza
safari zake kwa mara ya kwanza Juni 2015.
Pia, ndege hiyo inatoa huduma Singapole, Washington DC, Zurich na Dusseldorf.
Vilevile Shirika linatarajia kuanzisha huduma hiyo Istabul, Johnnesburg na Shangai kwa kipindi hiki kilichobaki kwa mwaka huu.
Aidha
ndege za Boing 787 Dreamliner inategemewa kuwa ndizo ndege zikazotoa
huduma kwa miaka michache ijayo katika shirika hilo kutokana na ubora
wake na teknolojia yake ya kisasa.
Wanaotumia
ndege ya Dreamliner watafurahia usafiri huo kutokana na kuwa na
madirisha makubwa, hewa nzuri ya ndani ya ndege, mandhari mazuri pamoja
na vifaa vilivyopo ndani vyenye kutumia teknolojia ya kisasa.
Safari za Abu Dhabi-Perth:
Namba ya Ndege
|
Inakotoka
|
Kuondoka
|
Mahali/kwenda
|
Kuwasili
|
Siku
|
Ndege
|
EY486
|
Abu Dhabi
(AUH)
|
4:30 usiku
|
Perth
(PER)
|
7:50 mchana next day
|
Daily
|
B787-9
|
EY487
|
Perth
(PER)
|
11:00 jioni
|
Abu Dhabi (AUH)
|
6:25 mchana
next day
|
Daily
|
B787-9
|
Muhimu: Muda wa kuondoka na kuwasili umewekwa kwa masaa ya eneo husika.
SHARE









No comments:
Post a Comment