Stephen
Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini jinsi Rais Obama
anavyoelekezwa namna ya kutumia simu kuendesha mashine hiyo katika
Onyesho la ubunifu wa kisayansi ambalo lilifadhiliwa na Rais Barack
Obama katika Ikulu ya Rais ( White House Science Fair 2016)
April 13,
2016, Rais wa Marekani, Barack Obama, alifadhili onyesho la mwisho
katika utawala wake, onyesho lililohusu ubunifu katika Nyanja za sayansi
ambalo limewahusisha wanafunzi kuanzia shule za awali, msingi hadi za
sekondari kutoka States mbalimbali za Marekani.
Kwa miaka
sita tangu mwaka 2010, Kiongozi huyo wa Marekani amekuwa akifadhili
onyesho hilo lijulikanalo kama White House Science Fair ambalo limekuwa
likifanyia katika Ikulu yake (White House) lengo likiwa ni kuhamasisha
wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, hisabati, teknolojia na ufundi (
STEM)na hivyo kuibua vipaji vya ubunifu m iongoni mwa wanafunzi ( young
inventors).
Katika
onyesho hilo la Aprili 13 jumla ya wanafunzi 130 walishiriki baada ya
kukidhi vigezo vya kuingia katika onyesho hilo. Miongoni mwa wanafunzi
waliopata fursa hiyo adhimu ya kushiriki baada ya kukidhi vigezo ya
ubunifu wao ni mwanafunzi mtanzania Stephen Wilfred Mwingira ambaye
pamoja na wenzake wawili Armo Halwah na Wendy Ni wanaosoma Baruch
College Campus High School ya jijini New York, wamebuni kifaa cha
gharama nafuu (vacuum cleaner) kinachoweza kutumika katika kusafisha
njia za reli za chini ya ardhi ( Subways).
Stephen
Mwingira na timu yake, walipata fursa ya kuelezea na kuonyesha mbele ya
Rais Obama namna gani kifaa walichobuni ( Vacuum Cleaner) kinavyoweza
kufanya usafi kwa kufungwa kwenye treni na hivyo kusaidia katika
kuzifanya njia za treni ( subways) kuwa katika mazingira ya usafi na
hivyo kupunguza gharama za usafishaji.
Katika
miaka sita tangu Rais Obama ambaye yeye binafsi amejipambanua kama
mpenzi na shabiki mkubwa wa sayansi na ubunifu, onyesho hilo limekuwa
motisha na kivutio kikubwa kwa walimu, wanafunzi, wafadhili na wataalamu
waliobeba katika masuala ya sayansi, teknolojia na hesabu.
Kila
mwaka State dining room ya Ikulu hugeuzwa kuwa eneo la maonyesho ambapo
wanafunzi hujipanga na kuonesha vifaa walivyobuni au kutoa maelezo ya
kisayansi ya namna ya kutatua tatizo Fulani kwa kutumia teknolojia
nafuu.
Katika
kutambua mchango wa Rais Barack Obama katika kuwahamasisha wanafunzi
kupenda masomo ya sayansi, Ikulu ya White House imetangaza kwamba
Kampuni ya Oracle inayojihusisha na masuala ya teknolojia ya Komputa
katika miezi kumi na nane ijayo itawekeza dola za kimarekani 200 milioni
kwaajili ya masomo ya sayansi ya computa kwa wanafunzi wa kimarekani.
Katika
maelezo yake kwa vyombo vya habari kabla na baada ya kuhitikishwa kwa
onyesho lake la mwisho, Rais Barack Obama amesema, mara zote ambazo
ameshiriki kujionea ubunifu wa vijana hao wadogo na wenye kiu na ari ya
kuibua mambo mapya, amekuwa akijifunza kitu kipya na mara zote amejiona
kama anayepungukiwa na kitu kutokana kile anachojifunza kutoka kwa
wanafunzi hao.
“Nimeweza
kujionea ubunifu wa hali ya juu, kiu, na hamu ya watoto na vijana wetu
wataalamu wa kesho wa taifa letu la marekani. Ipo siku huko mbeleni
nitajivunia pale ambapo miongoni mwa vijana wetu hawa watakapoweza
kubuni tiba ya kansa.
Nitaangalia
nyuma kwa fahari kubwa kwamba niliwawezesha vijana hawa kuibua vipaji
vyao ”. Akasema Rais Obama kwa furaha huku akiwashukuru wale wote ambao
kwa miaka sita mfululizo wamewezesha kwa namna moja ama nyingine
kufanyika kwa onyesho hilo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment