
Uongozi
wa Young Africans ya Dar es Salaam, umekamilisha maandalizi yote muhimu
ya mchezo dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola wa kufuzu hatua ya
makundi Kombe la Shirikisho la Barani Afrika utakaofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam leo Jumamosi Mei 7, saa 10:00 jioni.
Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana ukisimamiwa na kamishna kutoka Ethiopia.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry
Muro ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa Jukwaa la VIP “A” kuwa ni Sh
30,000; VIP “B” na “C” Sh 20,000 wakati jukwaa la viti Rangi ya chungwa
ni Sh 7,000 wakati mzunguko wa viti vya bluu na kijani ni Sh 5,000.
Kwa
mujibu wa Muro, Yanga itawakosa wachezaji mahiri wawili, Donald Ngoma na
Thaban Kamusoko ambao watatumia mchezo huo kutumikia adhabu ya kadi
mbili za njano walizoonywa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika
kabla ya kushuka kucheza Kombe la Shirikisho.
“Tunawaomba
wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga tujitokeze kwa wingi leo
kuishangilia timu yetu kwa nguvu na kasi kubwa,” amesema Muro ambaye
alitumia nafasi hiyo kutamba kwamba Yanga ilisajili wachezaji 24 kwenye
michuano inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) (P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment