Michael Sandford
Mwanamume
mmoja raia wa Uingereza anayetuhumiwa kwa kupora bunduki ya afisa mmoja
wa polisi katika mkutano wa kisaiasa wa Donald Trump, amewaambia
wapelelezi wa Marekani kuwa, alitaka kumuua kwa kumpiga risasi na
kumuuwa mgombea huyo wa kiti cha Urais wa chama cha Republican.
Kwa mjibu
wa stakabadhi za mahakama, Michael Sandford anasema kuwa aliendesha
gari hadi Las Vegas akiwa na nia ya kumpiga risasi Bw Trump siku ya
Jumamosi.Awali Donald Trump alimtimua Maneja wake wa kampeni Corey
Lewandowski kwa kutofautana naye katika kauli zake.
Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amemlaum Trump kwamba kauli zake ni za hatari. BBC
SHARE








No comments:
Post a Comment