Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu (katikati) na Mhariri wa Mawio, Simon
Mkina (wa poli kutoka kushoto mwenye miwani) na mchapishaji wao Ismail
Mahboob (wa tatu kutoka kushoto mbele).
MBUNGE wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mhariri wa Mawio, Simon Mkina na
mchapishaji wao Ismail Mahboob jana wamepandishwa tena mahakamani
Kisutu, Dar kwa uchochezi.
Kwenye
shitaka hilo, Lissu pamoja na washitakiwa wenzake wanadaiwa kufanya
makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchochezi kupitia Gazeti la Mawio
la Januari 14, 2016.
Kwenye
gazeti hilo lililoandikwa kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’
Lissu alinukuliwa kama mchangiaji wa gazeti hilo ambapo tayari limefutwa
na serikali.
Hii ni mara ya pili washitakiwa hao kupandishwa kizimbani. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 11, 2016.GPL(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment