Maafisa wa polisi wa Orlando
Magaidi
siku zote wana angalau malengo mawili pindi wanapofanya mashambulizi.
Wanakusudia kuwaua watu wanaowalenga, na pia kuharibu kabisa maeneo ya
wazi ya kijamii. Haya ni maoni ya mwandishi wa DW Washington, Ines Pohl
Shambulizi
katika klabu ya usiku huko Orlando, Marekani lililowaua kiasi ya watu
50, ni janga ambalo sio tu la kutisha, bali pia la hatari. Katika mwaka
huu wa uchaguzi, mshambuliaji huyo wa Orlando huenda akafanikiwa kwa
malengo hayo.
Shambulizi
hilo la Orlando limetokea wakati ambapo Marekani imejikuta iko katikati
mwa mtihani muhimu. Marekani ambayo ndiyo kwanza iko mwanzoni mwa
mapambano kuhusu swali la nani ataingia katika Ikulu ya White House kama
rais ajaye wa nchi hiyo. Shambulizi hilo limetokea wakati ambapo
uchaguzi wa urais umeanza kupamba moto.
Muda
mfupi baada ya shambulizi kutokea, wafuasi wa Donald Trump, wameonyesha
jinsi gani wangeweza kumaliza kitendo hiki cha ugaidi. Wameandika katika
mtandao wa kijamii wa Twitter wakimpongeza Trump kuhusu msimamo wake wa
kupambana na Uislamu katika mtazamo dhahiri wa dini ya mshambuliaji.
Msimamo wa Hillary kutumiwa dhidi yake
Hatua ya
Hillary Clinton kuwa karibu na kuonyesha mshikamano na Waislamu, ni
suala ambalo watalitumia dhidi yake. Watautumia mwanya wa hofu ya watu
kumuweka kileleni mgombea wao. Kwa mwaka huu hasa, Wamarekani wengi
wanaonekana kukabiliwa na vuguvugu la aina hii la kisiasa.
Wakati
Donald Trump aliposema anataka kuifanya Marekani kuwa nzuri tena,
akilini mwake alikuwa na nchi ambayo atakuwa kama mwenyeji mbabe. Hatua
hiyo ni kile kilicho nyuma ya mpango wake wa kupiga marufuku kwa muda
Waislamu kuingia Marekani, wasiwasi kuhusu jaji mwenye asili ya Mexico
au udhalilishaji dhidi ya wanawake.
Mashambulizi
ya kigaidi yanaweka changamoto kubwa katika kila jamii ya wazi.
Mashambulizi hayo yanawalazimisha kujiuliza maswali magumu kuhusu
thamani ya uhuru wao. Ni wajibu mgumu kwa wanasiasa na watu kukabiliana
kwa utulivu na kuwa na mtazamo wa pamoja kuhusu hisia ya chuki na kisasi
ambavyo vinaonyeshwa kupitia ugaidi. Rais Francois Hollande wa
Ufaransa, alifanikiwa kwa kufanya hivyo, baada ya mashambulizi ya Paris.
Aliwaongoza vyema watu wake.
Lakini
kampeni za uchaguzi zinaanza nchini Marekani, mambo ambayo dunia
haijawahi kamwe kushuhudia. Je Marekani ya 2016 itafanikiwa kuepukana na
mtego uliowekwa na magaidi, katika kile ambacho kinaonekana kukosekana
kwa uhuru kinachotarajiwa kufanywa na Waislamu wenye itikadi kali? Au
itaweza kuitetea ndoto ya Marekani, ambayo kwa kiasi kikubwa imejengwa
katika jamii ya wazi ya wahamiaji? Uwezekano ni kwamba ghadhabu ya
kipofu itashinda.DW
SHARE
No comments:
Post a Comment