Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu akipokea msaada
uliotolewa na Bodi ya TPDC (kushoto). Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
TPDC Balozi Dkt. Ben Moses msaada ambao unalenga kuwasaidia kurekebisha
makazi ya waathirika wa tetemeko hilo lililoukumba mkoa huo.Picha na
Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu (kulia) akimshukuru
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Kamugisha Kazaura
(kushoto) mara baada ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya saruji ambayo
ni sawa na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10.
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
Wafanyakazi
na Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wametoa
msaada wa Sh. milioni 20 kusaidia kununua vifaa vya ujenzi kwa
waathirika wa tetemekola ardhi mkoani Kagera.
Akikabidhi
msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa huo Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu,
Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC Balozi Dkt. Ben Moses amefafanua kuwa msaada
huo unalenga kuwasaidia kununua mabati na saruji kwa waathirika wa
tetemeko hilo lililoukumba mkoa huo.
“Sisi
TPDC tunatoa msaada wetu kama sehemu ya Watanzania na tatizo hili ni
letu sote na Watanzania ni wamoja” alisema Dkt. Moses.
Kwa
upande wake Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewashukuru TPDC kwa mchango
wao na kubainisha kuwa hakuna kitu kidogo katika kutoa na kuwahakikishia
wadau wote wanaotoa michango yao kuwa misaada hyote inayotolewa
itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na itasaidia kuwarudishia makazi
waathirika wa tetemeko hilo.
Aidha,
Mkuu huyo wa mkoa amewataka watu wote wenye mapenzi mema kuendelee
kuwachangia waathirika wa tetemeko hilo na waige mifano ya watu na
taasisi mbalimbali wanaoendelea kutoa misaada kwa mkoa wa Kagera ili
kuwarudishia makazi wananchi walioathirika maafa hayo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Kapuulya Musomba amesema kuwa huo
sio mwisho wao katika kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi, bali
wanaendelea kuwahamasisha wadau wa mafuta na gesi yakiwemo makampuni ya
ndani na nje ya nchi ili kuwafanya wananchi waweze kuendelea na kazi zao
za kila siku kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Wakati
huo huo Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) nao wametoa msaada wa mifuko
saruji 600 ambayo ni sawa na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10
ikiwa ni mchango wa wa kampuni hiyo katika kuwashika mkono na kuwafuta
machozi wananchi wa Kagera. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment