TRA

TRA

Tuesday, February 28, 2017

ASKOFU GADI AMPONGEZA RAIS DK. MAGUFULI KUMTEUA KAMISHNA WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA, AMUOMBEA PAMOJA NA NCHI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Askofu Ernest Sumisumi (wa pili kushoto) wa Kanisa la Baptist akiiombea ramani ya Tanzania pamoja na picha ya Rais Dk. John Magufuli.
Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi na Askofu Filbert Mbepera (kuli), wakiyabariki mafuta ya kupaka picha ya Rais, Dk. Magufuli.
Askofu Hezron Mwamsemba wa Kanisa la Baptist akiipaka mafuta picha ya Rais Dk. John Magufuli.
Maaskofu wa madhehebu mbalimbali wa dini ya Kikristo, wakiinyanyua juu picha ya Rais Magufuli, baada ya kuipaka mafuta na kuiombea.
Askofu John Sambuki (wa pili kulia) wa Victory Gospel Assemble a.k.a Furahini Katika Bwana, akiiombea bendera, wakati wa hafla hiyo.
Maaskofu na baadhi ya watumishi wa madhehebu hayo ya dini ya Kikristo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maombi hayo.
Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi  akizungumza na waandishi wa habari wakati madhehebu mbalimbali hapa nchini walipomuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nchi, pamoja na kumpongeza kwa kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dar es Salaam leo. Kushoto ni Askofu Hezron Mwamsemba wa Kanisa la Baptist jijini na katikati ni Askofu Ernest Sumisumi wa kanisa hilo.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi  wakati alipokuwa akizungumza.
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo, wakiongozwa na Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi (katikati), wakiimba wimbo wa amani wakati wa kumuombea Rais Dk. Magufuli na Taifa.
Askofu Filbert Mbepera (wa pili kuli) wa Kanisa la EAGT, akiombea amani nchi.


Na Lilian Lundo – Maelezo
ASKOFU wa Good News  for All Ministry  Dkt. Charles Gadi  kwa niaba ya dini na madhehebu mbalimbali hapa nchini wamempongeza  Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Dkt. Gadi ametoa pongezi hizo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

“Tunamshukuru Mungu kwa kumuinua Rais ambaye ameonyesha nia na kuwa mstari wa mbele  kupigana na biashara hiyo haramu, ni ukweli usiopingika kwamba tatizo la dawa  ya kulevya ni kubwa na lenye madhara makubwa sana kwa watanzania  wengi haswa vijana ambao ni nguvu kazi  ya Taifa,” alifafanua Dkt. Gadi.

Aliendelea kwa kusema kuwa, Vijana wengi wamepoteza maisha , kuharibika akili, kupata magonjwa ya kuambukiza, kupoteza malengo ya kimaisha kwa sababu ya dawa hizo. Vile vile dawa hizo zimeleta fedheha kwa Taifa kutokana na Vijana wengi wa Kitanzania kuwepo katika magereza mbalimbali Duniani huku wengine wakisubiri  adhabu  ya kunyongwa.

Aidha amempongeza Rais Dkt. Magufuli kwa kuimarisha Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa  kumteua Kamishna ambaye atasimamia Mamlaka hiyo na anaamini kwamba kwa neema ya Mungu ataweza kumsaidia kikamilifu  Rais Magufuli katika kutimiza azma yake ya kukomesha  biashara hiyo.

Wakati huo huo, Dkt. Gadi amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuianzisha vita hiyo dhidi ya matumizi ya dawa kulevya katika mkoa wa Dar es Salaam. Vile vile amewapongeza waandishi wa habari na vyombo mbalimbali vya habari kwa kutoa habari zinazosaidia katika upambanaji wa  biashara hiyo.

Dkt. Gadi amewataka viongozi wa Dini kuungana bega kwa bega na Rais Magufuli kwa kuendelea kutoa maadili kwa vijana ili kuepukana na uovu wa dawa za kulevya nchini.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger