Malaysia imemuita balozi wake nchini Korea Kaskazini kufuatia tofauti zilizojitokeza kati ya mataifa hayo mawili kutokana na kifo cha nduguye Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kilichotokea uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
Nchi hiyo pia imesema kuwa imemtaka balozi wa Korea Kaskazini ametuhumiwa na serikali ya Malaysia kutokana na shutuma zake dhidi ya nnchi hiyo wiki iliyopita kutokana na kifo hicho.Nduguye Rais wa Korea Kaskazini inadaiwa kuwa aliuawa kwa sumu na Malaysia inaendelea na uchunguzi japo kuwa Korea Kaskazini inahitaji kurejeshewa mwili huo na kwamba haihitaji uchunguzi wowote ikiwepo upasuaji kufanyika.
Hata hivyo Malaysia imesisitiza itaendelea na uchunguzi na kwamba ina mamlaka ya kufanya uchunguzi huo kwa kuwa alifia katika ardhi ya nchi yao lazima wafanye uchunguzi na hakuna wa kuwazuia.
SHARE
No comments:
Post a Comment