Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Ali Hapi amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
kuhakikisha anapeleka Mameneja pamoja na mashine za
kielektronic(EFD),kwenye masoko kwa lengo la kudhibiti upotevu wa mapato
unaoendelea.
Ametoa
agizo hilo jana alipokuwa akisomewa taarifa ya mapato na matumizi ya
Masoko na Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama Bi. Elizabeth Minga ambapo
ilionesha upotevu mkubwa wa fedha kwenye masoko hasa soko la wamachinga
lililoko Mwenge.
Amesema fedha nyingi zinapotea kutokana na kutokuwepo utaratibu mzuri wa kukusanya mapato kwenye masoko.
Katika
hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amepiga marufuku uanzishwaji wa
vikundi vya kiholela vya kusimamia masoko ili kudhibiti upotevu wa
mapato unaoendelea.
Kijitonyama
ni Kata ya nne kati ya Kata kumi za awamu ya pili zinazotembelewa na
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo
pamoja na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akiongea na Wamachinga wa soko la Mwenge ,Jijini Dares salaam
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akiendelea na ukaguzi soko la Mwenge, Jijini Dares salaam
SHARE
No comments:
Post a Comment