Rais
Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu Dkt.
Jakaya Kikwete akikaribishwa na Rais Alassane Ouatara wa Ivory Coast
jijini Abidjan katika Ikulu ya nchi hiyo.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi ripoti ya ‘Kizazi cha Elimu’ Rais Allasane Ouatarra wa Ivory Coast
Rais
Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya
mazungumzo na Rais Alassane Ouattara. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa
nchi hiyo Mhe. Daniel Kablan Duncan.
Rais
MStaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa
Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika jijini Abidjan
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwasainia autograph watoto waliomtembelea hotelini kwake jijini Abidjan.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia mazungumzo na baadhi ya
watoto wa Watanzania waishio Ivory Coast waliomtembelea hotelini kwake
Abidjan.
Rais
Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 23Februari 2016 amekutana na kufanya
mazungumzo na Rais wa Ivory Coast, Mhe. Alassane Ouattara katika Ikulu
yake jijini Abidjan.. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu wa
Rais, Waziri wa Fedha na Waziri wa Elimu.
Katika
mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji
wake Rais Ouattara wamezungumzia hali ya elimu bara la Afrika na Ivory
Coast kwa ujumla na haja ya kufanya mageuzi makubwa katika elimu ili
kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea.
Rais
Mstaafu Kikwete amempongeza Rais Outtara kwa jitihada kubwa anayoifanya
kuinua elimu nchini mwake. Kwa mujibu wa utafiti wa Kamisheni, Ivory
Coast iko katika nafasi nzuri ya kufikia viwango vya juu vya ubora wa
elimu vya nchi zilizoendelea iwapo itaongeza juhudi ya kufanya mageuzi
kulingana na mapendekezo ya Kamisheni hiyo.
Rais Outtara
amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete azma ya nchi
yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini mwake.
Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha
mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.
Akiwa
jijini Abidjan, Rais Mstaafu ametembelewa na viongozi wa Watanzania
wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika na Watoto wa Watanzania
hao ambao walitaka kujua kuhusu masuala ya uongozi na maisha baada ya
kustaafu.
SHARE
No comments:
Post a Comment