Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa
kukubali kuendelea kufadhili miradi ya maendeleo ya kipaumbele hususani
ya ujenzi wa barabara na usafirishaji wa umeme ili kufungua fursa za
kiuchumi katika kanda ya Magharibi.
Dkt.
Mpango ametoa shukrani hizo alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12
wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB),
jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ameiomba Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na
hatimaye kutoa fedha ili utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kuanza
mapema iwezekanavyo.
Amesema
kuwa Benki hiyo iliahidi kutoa fedha ili kujenga barabara ya Nyakanazi,
kupitia Kibondo, Kasulu hadi Manyovu, kwa kiwango cha lami na kwamba
mradi huo ukipatiwa fedha na kukamilika kwa wakati kutasaidia kuchochea
biashara ya wakazi wa maeneo hayo na Nchi jirani ya Burundi.
Pia
mradi wa North – West grid wa kusafirisha Nishati ya Umeme kutoka
Shinyanga hadi Mbeya kupitia Kigoma Katavi na Rukwa. Mradi huu
utawezesha Mikoa ya ukanda wa Magharibi kupata Nishati ya uhakika ya
umeme na kufungua fursa za Maendeleo mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa
Viwanda vidogo na vya kati.
“Katika
kikao hicho tumewaeleza Wakurugenzi hao wa AfDB hatua mbalimbali ambazo
Serikali inazichukua katika kutatua changamoto ya Miundombinu ya Umeme
na Barabara, kupanua fursa za Ajira, na kuharakisha maendeleo ya ukuaji
wa Sekta ya Kilimo ambayo inategemewa na wananchi wengi” Alifafanua
Waziri Mpango.
Aidha
amewaeleza wageni juu ya jitihada za Serikali ya Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli za kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, kupambana
na rushwa na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Waziri
Mpango ametumia fursa hiyo kuomba AfDB kusaidia kujenga uwezo wa
Tanzania kukabiliana na majanga yakiwemo ya matetemeko ya ardhi, ajali
kubwa za majini na kwenye migodi. Maeneo mengine ambayo AfDB imeombwa
kuisaidia Tanzania ni uvunaji wa rasilimali za bahari (blue economy),
kuelekeza mitaji katika Sekta ya kilimo na kukabiliana na athari za
mabadiliko ya Tabia nchi.
Naye
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
ameipongeza Benki ya AfDB kwa kuwa mdau mkubwa wa Maendeleo ya nchi za
Afrika na hasa Tanzania kwa kuwa imekuwa mnufaika mkubwa wa program/
miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo.
Amewataka
wananchi kutoa ushirikiano kwa wageni hao watakapokuwa wakitembelea
miradi mbalimbali inayogharamiwa na AfDBi katika siku takribani tano
ambazo watakuwepo nchini.
Kwa
upande wa Wakurugenzi Watendaji wa AfDB wanaoziwakilisha nchi zao,
wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Elizabeth
Mmakgoshilekethe, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa mafanikio
ya kiuchumi kwa kuwa Tanzania imekuwa na viashiria vingi ambavyo
vinaonesha uchumi wa Taifa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine
katika bara la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
Aidha
wameitaka Tanzania kuendeleza jitihada za kupambana na Umaskini hasa
katika maeneo ya vijijini na kuongeza fursa za ajira ili kuharakisha
maendeleo. Pia wameipongeza Serikali kwa mikakati waliyonayo kupitia
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa miaka mitano kwa kuwa unaendana na
vipaumbele vya Benki hiyo.
Benki
hiyo imeitaka pia Tanzania kushiriki na kuchangamkia fursa za miradi ya
kikanda hasa katika Nishati ya Umeme, Barabara na Reli na pia
kuhakikisha utawala bora.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa akielezea umuhimu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati akizungumza na Wakurugenzi 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki hiyo Mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa akielezea umuhimu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati akizungumza na Wakurugenzi 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki hiyo Mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
Maafisa waandamizi
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa Makini Maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha
nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (hayupo) pichani wakati wa
mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango
(Mb) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth
Mmakgoshilekethe (kulia) akiipongeza Serikali kwa kuweka vipaumbele vya
maendeleo vinavyoendana na vile vya Benki ya Maendeleo ya Afrika katika Mkutano
na Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kushoto) katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa
Wakurugenzi anayeiwakilisha nchi yake katika Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) akipongeza juhudi za Serikali katika kuwataulia wananchi wake matatizo
ya kiuchumi wakati wa Mkutano kati ya Wakurugenzi hao na Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo wakati wa
Mkutano wake na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya
Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (kulia) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), akiongoza mkutano ulio wakutanisha Wakurugenzi
Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania huku ahadi zilizotolewa na Benki hiyo
zikijadiliwa katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), (katikati) na Kiongozi wa Ujumbe wa AfDB, Bi. Elizabeth
Mmakgoshilekethe, kutoka Afrika Kusini (wa pili kushoto), wakiwa katika picha
ya pamoja na Wakurugenzi wengine wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya AfDB
baada ya kumalizika kwa Mkutano katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango,
jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kulia) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
(Mb) (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kutoka
Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth
Mmakgoshilekethe (katikati) wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa
Mkutano kuhusu Hali ya uchumi nchini Tanzania katika ukumbi wa
Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment