Chemba
ya biashara, viwanda na kilimo( TCCIA) inatarajia kufanya ziara ya
kibiashara nchini Italy na Uturuki ambapo Chemba inapenda kuwakaribisha
wafanyabiashara walio wanachama na wasio wanachama kuungana nasi kwenye
mkutano huu wa wawekezaji. Chemba inawakumbusha kwamba, imabaki siku
moja kwa wafanyabiashara wa Italy kuthibitisha ushiriki wao ambapo
mwisho ni tarehe 3 March 2017. Kwa 3wafanyabiashara wa Uturuki wana muda
mrefu ambapo muda wa mwisho wa kuthibitisha ushiriki wao ni tarehe 30
March 2017. Ziara hii inatarajia kufanyika mwanzoni mwa mwezi May.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Ndugu Gotfrid
Muganda alisema “Lengo kubwa la ziara hii ni kuwawezesha
wafanyabiashara wa Tanzania kutanua wigo wa masoko na fursa za
kibiashara na kubadilishana ujuzi”. Akizungumza juu ya ziara hiyo
Mkurugenzi wa EAG Group ambao ni washauri wa biashara na masoko wa TCCIA
Imani Kajula alisema “Ukuzaji wa masoko ya nje ni mkakati endelevu
ambao sio tu utaongeza soko nje lakini pia kuleta urari mzuri wa
biashara na hivyo kusaidia kuimarisha thamani ya shilingi”. Aliwaambia
wafanyabiashara ambao ni wanachama na wasio wanachama wanakaribishwa
kijiandikisha ambapo mwisho kwa wanaoenda Italy ni tarehe 3 March
2017..
SHARE
No comments:
Post a Comment