• About
  • Services
  • Products
  • Blog
  • Contact Us

NCHI YANGU

Menu
  • Home
  • Lifestyle
    • Sub Menu 1
    • Sub Menu 2
    • Sub Menu 3
  • Sports
    • Sub Menu 1
      • Sub Menu 1
      • Sub Menu 2
      • Sub Menu 3
    • Sub Menu 2
    • Sub Menu 3
  • Post
  • Fitness
  • Music
  • Travel
  • Politics
  • Beauty

TRA

TRA

Monday, April 24, 2017

Home > > Uchaguzi Ufaransa: Emmanuel Macron na Marine Le Pen waongoza duru ya kwanza

Uchaguzi Ufaransa: Emmanuel Macron na Marine Le Pen waongoza duru ya kwanza

at 2:27 AM
Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Mgombea urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa nchi hiyo, huku dalili zikionyesha, baada ya wiki mbili atapambana katika duru ya pili na Marine le Pen ambae ni mgombea wa chama chenye mrengo wa kulia cha National Front. Aboubakar Famau na taarifa zaidi:

Macron mwenye umri wa miaka thelathini na tisa na aliyewahi kuwekeza katika sekta ya benki, hajawahi kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kabla, amesema, shaka, hofu na hamu ya mabadiliko aliyokumbana nayo katika kampeni ndio iliyosababisha wapiga kura kuacha vyama vikuu vya kisiasa ambavyo vimekuwepo uongozini kwa miaka thelathini.




                                      Emmanuel Macron
"Nimesikia katika miezi iliyopita na leo tena, shaka, hasira na uoga waliokuwa nao wafaransa. Na hamu ya mabadiliko. Hiki ndicho kilichowasukuma kuacha vyama vikuu viwili vilivyotawala kwa zaidi ya miaka thelathini.")
Ameongeza kusema kazi yake hivi sasa ni kuipatanisha nchi na kuunganisha nguvu kwa ajili ya duru ya pili ya uchaguzi."wiki mbili kuanzia sasa, nataka niwe rais wenu. (CROWD CHEERING) Rais wa raia wote wa ufaransa. Rais wa wapenda nchi dhidi ya vitisho vya wanaotaka kujitenga.")
Kwa upande wake, Le Pen ameyaelezea matokeo hayo kuwa ni ya kihistoria. Huku akijiita kuwa yeye ni ndio chaguo la wafaransa na kusema kuwa muda umefika wa kuwabadilisha watu.
"Wakati umefika wa kuwaweka huru raia wa ufaransa na jamii yote wa rais wa Ufaransa bila kusahau marafiki zetu walio nje ambao wameniamini na naona fahari kwa imani walioonyesha kwangu.")
  • Uchaguzi Ufaransa 2017: Wanaowania ni akina nani?
Rais wa ufaransa amempigia simu bwana Macron na kumpongeza, bila kuonyesha kumuunga mkono rasmi.
 
                                      Wafuasi wa Bw Macron wakisherehekea...

Mmoja wa wasaidizi amesema haikuna vigumu kujua chaguo lake kati ya waziri aliyefanya kazi nae na mwakilishi mwenye mrengo wa kulia.Francois Fillon ambae ni mgombea wa mrengo wa kati, na aliyewahi kuwa waziri mkuu, ambae pia aliwahi kukabiliwa na tuhuma za ufisadi, wakati akiwahutubia wafuasi wake amesema atampigia kura Macron.
Wakati hayo yakijiri, kumetokea vurugu katikati mwa jiji la Paris zilizohusisha vijana wenye mrengo wa kushoto ambao hawakufurahishwa na ushindi wa Le Pen.
Polisi walipambana nao kwa kuwapiga viboko.Vile vile kumekuwa na maandamano magharibi mwa mji wa Nantes.
Tayari viongozi mbali mbali wa nchi za ulaya wameanza kuonyesha kumuunga mkono Macron.
Msemaji wa Chancellor wa ujerumani Angela Merkel amemtakia kila la heri, na kusifu msimamo wake kuunga mkono Umoja wa Ulaya.


                Wafuasi wa Marine Le Pen nao wakisherehekea
  
Hata hivyo, Le Pen pia amepata kuungwa mkono kutoka jamii ya kimataifa ambapo mwenyekiti wa kamati ya uhusiano wa mambo ya nje katika bunge la Urusi, amesema Le Pen ndio tegemeo pekee la mabadiliko.

Unknown

Author: Unknown

SHARE
  • Share
  • Tweet
  • Share
  • Pin
  • Share
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Fourni par Blogger CodeEnvoyer par emailBlogThis !Partager sur TwitterPartager sur FacebookPartager sur LinkedInÉpingler sur PinterestPartager sur StumbleUponVoter pour cet article sur HelloCoton

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Tupate kupitia Facebook

Popular Posts

  • Wataalamu: Iraq bado ina changamoto
    Iraq bado ina changamoto nyingi licha ya ushindi wa majeshi yake dhidi ya kundi la wapiganaji wanaojiita Dola la Kiislamu, IS, ilioup...
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YATEMBELEA HIFADHI YA MAZINGIRA ASILIA ULUGURU
    Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ard...
  • Jaribio la Korea Kaskazini lashtua dunia
    Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis amesema Marekani itajibu kwa njia mbali mbali kitisho chochote kutoka kwa Korea Kaskazini ...

Popular Posts

  • Wataalamu: Iraq bado ina changamoto
    Iraq bado ina changamoto nyingi licha ya ushindi wa majeshi yake dhidi ya kundi la wapiganaji wanaojiita Dola la Kiislamu, IS, ilioup...
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YATEMBELEA HIFADHI YA MAZINGIRA ASILIA ULUGURU
    KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YATEMBELEA HIFADHI YA MAZINGIRA ASILIA ULUGURU
    Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ard...
  • Jaribio la Korea Kaskazini lashtua dunia
    Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis amesema Marekani itajibu kwa njia mbali mbali kitisho chochote kutoka kwa Korea Kaskazini ...
  • Dalili tano za wanawake wanaochepuka |
    ...
  • WALIOSOMA KILAKALA SEKONDARI WACHANGISHANA FEDHA , WAKARABATI JENGO LA ZAHANATI , WANUNUA SHUKA NA MAGODORO , MADAFTARI
    WALIOSOMA KILAKALA SEKONDARI WACHANGISHANA FEDHA , WAKARABATI JENGO LA ZAHANATI , WANUNUA SHUKA NA MAGODORO , MADAFTARI
    WAHITIMU waliosoma Shule ya Sekondari  Kilakala   , iliyopo mkoani Morogoro wameombwa kujitokeza kuunga mkono mpango wa Serikali wa...
  • WAKANDARASI NCHINI WAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI
    WAKANDARASI NCHINI WAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI
      Picha ikimuonyesha Mkandarasi kutoka Kampuni ya Caberisa Co.Ltd Bernad Mgohamwende ambaye anajenga barabara kw...

Pages

  • Home
  • About Us
  • Contat Us
 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger