Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
ameiagiza migodi mikubwa nchini Tanzania kuanzisha programu maalum kwa
ajili ya kutoa elimu ya afya na usalama kwa wachimbaji wadogo wa madini
ili kuepuka ajali zinazotokea kwenye maeneo ya migodi.
Waziri Mhagama ametoa agizo hilo leo
Ijumaa Aprili 28,2017 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
mkoani Kilimanjaro wakati akikagua mabanda ya maonesho ya migodi
mbalimbali nchini ikiwemo inayomilikiwa na kampuni ya Acacia inayomiliki
migodi ya Bulyanhulu,Buzwagi na North Mara.
“Serikali imeridhishwa kuhusu namna
migodi mikubwa nchini inavyozingatia suala la usalama na afya mahali pa
kazi,migodi hii mikubwa inatakiwa kutengeneza program maalumu za
kufundisha migodi midogo midogo inayowazunguka ili watanzania wote
waweze kujua namna gani wanaweza kuwa salama katika shughuli za
uchimbaji madini”,alisema Mhagama.
“Tumekubaliana mwaka ujao kila mgodi utatoa taarifa namna gani kuwasaidia watanzania kuwa salama katika maeneo ya kazi”,alieleza Mhagama.
Akizungumza katika mabanda ya Kampuni ya
uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia inayomiliki migodi ya
Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara,Mhagama alieleza kufurahishwa kuhusu
namna kampuni hiyo inavyokusanya na kutumia takwimu za afya na usalama
mgodini.
Waziri Mhagama alikuwa mgeni rasmi katika siku ya Usalama na afya mahali pa kazi duniani kitaifa mkoani Kilimanjaro.
Nimekuwekea
hapa picha za matukio wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akitembelea
mabanda ya kampuni ya Uchimbaji madini ya Acacia
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akiwa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu katika viwanja vya Chuo Kikuu
cha Ushirika Moshi kwa ajili ya kuangalia vifaa vya kisasa vinavyotumika
katika uokoaji na namna mgodi huo unavyofanya katika kuhakikisha
wafanyakazi wao wanakuwa salama mgodini
Kulia ni Afisa Uhakiki wa Usalama mgodi
wa Bulyanhulu Amina Mohamed akimweleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista
Mhagama kuhusu namna wanavyokusanya takwimu za afya na usalama mgodini
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akiangalia vifaa vya kisasa vinavyotumika katika kutunza takwimu za afya
na usalama katika mgodi wa Bulyanhulu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akisisitiza maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu kuanzisha programu
maalumu ya utoaji elimu ya usalama na afya kwa wachimbaji wadogo wadogo
wa madini
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akizungumza na maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akiangalia kitabu maalumu kinachotumika kukusanya takwimu za afya na
usalama katika mgodi wa Bulyanhulu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akizungumza jambo na Kiongozi wa kitengo cha afya mgodi wa Bulyanhulu
Dkt. Kudra Said (kushoto).Katikati ni Afisa Mahusiano mgodi wa
Bulyanhulu Mary Lupamba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akifurahia jambo na maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu
Kulia ni Kiongozi wa Idara ya Mahusiano
ya Jamii mgodi wa North Mara Fatuma Mssumi akimkaribisha Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Jenista Mhagama katika banda la mgodi wa North Mara
Afisa Usalama na Afya mgodi wa North
Mara Alfred Mwema akielezea kuhusu namna mgodi huo unavyozingatia
masuala ya usalama mgodini.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akizungumza katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Kulia ni Dkt. Ludovick Silima kutoka
mgodi wa Buzwagi akionesha vifaa vya uokoaji vinavyotumiwa na mgodi huo
wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama alipotembelea banda la mgodi wa
Buzwagi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista
Mhagama akizungumza katika banda la mgodi wa Buzwagi. Aliyeshikilia
kipaza sauti ni Kaimu Mtendaji kutoka OSHA Hadija Mwenda
Kulia ni Mkufunzi Idara ya Uokoaji Mgodi wa Buzwagi Azael Kitange akionesha takwimu za afya na usalama za mgodi huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka kwa Mkufunzi Idara ya Uokoaji
Mgodi wa Buzwagi Azael Kitange.Kushoto ni Afisa Mawasiliano mgodi wa
Buzwagi Magesa Magesa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akiondoka katika mabanda ya kampuni ya Acacia inayomiliki migodi ya
North Mara,Buzwagi na Bulyanhulu.
SHARE
No comments:
Post a Comment