Bei ya mafuta
imeshuka kwa asilimia 5 licha ya mataifa yanayozalisha bidhaa hiyo
kukubaliana kupunguza kiwango cha uzalishaji kwa kipindi cha miezi
minane.
- Bei ya mafuta yaongezeka Tanzania
- Bomba la mafuta lalipuliwa Nigeria
- Sudan yaongeza bei ya mafuta kwa asilimia 30
Mafuta ghafi yalishuka kwa dola 2.60 hadi dola 51.36 kwa pipa siku ya Alhamisi na yalikuwa yamefika dola 51.47 Ijumaa alfajiri.
Waziri wa kawi nchini Saudia Khalid al-Falih aliyesimamia mkutano huo kama mwenyekiti mwenza na mwenzake wa Urusi Alexander Novak alisema: Tuliangazia vigezo kadhaa kutoka miezi 6, 9 na hadi 12 na pia tuliangazia uwezekano wa kupunguza uzalishaji huo kwa viwango vya juu.
Muungano wa mataifa ya OPEC na mataifa mengine 11 yasiozalisha mafuta ikiwemo Urusi, kwanza yalikubaliana kupugunza uzalishaji Disemba iliopita katika juhudi za kupiga jeki bei.
SHARE
No comments:
Post a Comment