Mkufunzi
wa Mafunzo, Wakili Dominic Ndunguru akielezea kuhusu ripoti ya utafiti
ya shirikisho la dini (Interfaith standing committee) iliyozinduliwa
Mwezi Mei mwaka 2017 kwa kuwashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge ya
Uchumi na Fedha inaliyoonyesha kuwa Tanzania kwa sasa inapoteza
takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia
misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata
utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za
ukwepaji kodi.
Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akiwasilisha
mada kuhusu mtazamo wa upatikanaji wa elimu nchini Tanzania wakati wa
Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi za Kiraia
waliokutana mkoani Singida yaliyofanyika kwa siku tatu.
Mdau wa Elimu kutoka asasi za kiraia, Lucy
Mkosamali akichangia mada ya umuhimu wa uwekezaji katika maendeleo ya
sekta ya elimu kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha
walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida
ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Mwenyekiti
wa Chama wa walimu Wilaya ya Singida, Bw. Hamisi Mtundua akichangia
mada kwa kutoa uzoefu wake kuhusu maslahi ya walimu na miundombinu ya
shule za vijijini kwenye mafunzo yaliyofanyika mkoani humo.
Afisa
Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akichangia mada
kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania
(CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida ulioandaliwa na
TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Washiriki
wa mafunzo wakifanya kazi za makundi kuhusu haki ya kupata elimu bora
kwenye mafunzo yalioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid
Tanzania.
Mwakilishi
wa Walimu Wanawake Chama cha walimu Manispaa ya Singida, Bi. Innosanta
Shayo akiwasilisha kazi ya kikundi cha Tano waliyokuwa wakijadili jinsi
ya mtoto kupata haki katika elimu.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu mkoani Singida wakifuatilia mafunzo
Mratibu
wa Elimu kata ya Mtinko akichangia mada ya haki za watoto mashuleni
pamoja na Umuhimu wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kuwekeza katika sekta
ya elimu kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Meneja
Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akiwaelekeza
washiriki wa mafunzo namna ya kuhamasisha haki za watoto mashuleni kwa
vitendo kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu
Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida
yalioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Afisa
Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akitoa uzoefu
wake kuhusu kuhamasisha haki za watoto mashuleni wakati wa elimu ya
vitendo kwenye mafunzo ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za utoaji wa
elimu bora hapa nchini mkutano huu uliowakutanisha wanachama wa chama
cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida
yalioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Washiriki
wa mafuzo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa
mafunzo yaliyofanyika kwa takribani siku tatu mkoani Singida
Mtandao
wa Elimu Tanzania (TENMET) kwa kushirikiana na ActionAid Tanzania
waliandaa mafunzo ya siku tatu kwa wanachama wa chama cha walimu na
asasi za kiraia za elimu mkoa wa Singida kuhamasisha upatikanaji wa haki
za mtoto shuleni na maendeleo ya sekta ya elimu kwa kushawishi serikali
kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kutumia rasilimali za
ndani.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja Mradi kutoka ActionAid Tanzania Karoli
Kadeghe alielezea katika bajeti ya elimu 2016/17, takribani bilioni 277
sawa na asilimia 31% ilitarajiwa kukusanywa kutoka kwa wahisani na
washirika wa maendeleo.
Hata hivyo, hadi kufikia mwezi Machi 2017, wahisani walikuwa wametoa kiasi cha shilingi bilioni 132 tu sawa na asilimia 47.6%. Alisisitiza kuwa ni vyema serikali iimarishe vyanzo vyake vya mapato vya ndani ili kuepuka aibu hii na sisi wadau wa elimu tunalo jukumu la kuisimamia serikali katika kutimiza wajibu wake.
Kila mtu akilipa kodi stahiki kadiri ya kile anachozalisha na pia serikali ikidhibiti mianya ya upotevu wa kodi, hata kodi ya PAYE itapungua na kumpa mwalimu ahueni katika makato hayo.
Hata hivyo, hadi kufikia mwezi Machi 2017, wahisani walikuwa wametoa kiasi cha shilingi bilioni 132 tu sawa na asilimia 47.6%. Alisisitiza kuwa ni vyema serikali iimarishe vyanzo vyake vya mapato vya ndani ili kuepuka aibu hii na sisi wadau wa elimu tunalo jukumu la kuisimamia serikali katika kutimiza wajibu wake.
Kila mtu akilipa kodi stahiki kadiri ya kile anachozalisha na pia serikali ikidhibiti mianya ya upotevu wa kodi, hata kodi ya PAYE itapungua na kumpa mwalimu ahueni katika makato hayo.
Mkufunzi
wa Mafunzo hayo Wakili Dominic Nduguru akiwasilisha mada juu ya ulipaji
wa kodi na Uwekezaji katika Elimu alitumia ripoti ya utafiti ya
shirikisho la dini (Interfaith standing committee) iliyozinduliwa Mwezi
Mei, 2017 kwa kuwashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi na
Fedha inaonyesha kuwa Tanzania kwa sasa inapoteza takribani dola bilioni
1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi,
uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza
kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi. Pia alidokeza
ripoti kadhaa zinazoonesha upotevu au ukwepaji wa kodi unaofanywa na
makampuni ya kigeni na wawekezaji wakubwa ambao unaathiri uwekezaji
katika uboreshaji wa huduma za jamii hususani sekta ya elimu.
Washiriki
wa mafunzo hayo kutoka chama cha walimu na asasi za kiraia za elimu
mkoa wa Singida wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Nguvu
ya kodi, haki za binadamu, haki ya watoto mashuleni, ushawishi na
utetezi wa maslahi ya walimu na haki za watoto, umuhimu wa ukusanyaji wa
kodi na rasilimali za ndani ili kuboresha miundombinu ya elimu na ubora
wa elimu.
Viongozi
na wanachama wa chama cha walimu pamoja na asasi za kiraia za elimu
mkoani Singida wameazimia kuyafanyia kazi mafunzo hayo na kuungana kwa
pamoja kwa kutengeza Mtandano wa Elimu Singida ili kushawishi mamlaka na
serikali kusimamia ukusanywaji wa mapato ya ndani ili kuboresha sekta
ya elimu. Washiriki walichagua uongozi wa mpito wa Mtandao wa Elimu
Singida na kuchagua taasisi ya Youth Movement for Change kama
sekretarieti ya muda.
SHARE
No comments:
Post a Comment