Wananafunzi
 wa Shule za Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, 
wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada
 na ziada, ili waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali.
 Wito
 huo umetolewa na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama 
Jacqueline Mengi, alipozungumza na wanafunzi, walimu na wajumbe ya 
Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho, wakati akizindua maktaba 
iliyokarabatiwa na mfuko huo. Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi 
kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi.
 Mkurugenzi
 wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi (kulia) akizungumza
 wakati wa uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya msingi 
Makumbusho jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz).
 Awali
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo, alitoa shukrani kwa 
Dr. Ntuyabaliwe Foundation kwa mchango wake wa vitabu kwa ajili ya 
maktaba hiyo, na kuomba kupatiwa mtaalam wa kutunza maktaba, ikiwezekana
 mwalimu mmoja akasomeshwe taaluma hiyo. Naye Afisa Taaluma Fatma Mwiru 
akimwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka waalimu 
kuwasaidia wanafunzi kupata vitabu mbalimbali, kwa kuwashirikisha wadau 
wa elimu, wachapishaji vitabu pamoja na wahisani. 
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akizungumza alipokuwa 
akimkaribisha Mama Jacqueline Mengi.[/caption] Aidha Mama Jaqueline 
Mengi amesema Dr. Ntuyabaliwe Foundation ilianzishwa mwaka jana ikiwa na
 lengo la kuchangia katika sekta ya elimu, ambapo iligundua shule nyingi
 za msingi zinakabiliwa na uhaba wa maktaba na vitabu. Shule ya Msingi 
Makumbusho inakuwa ya shule ya pili katika wilaya ya Kinondoni na ya 
kwanza katika kata ya Makumbusho, kusaidiwa ujenzi wa maktaba na msaada 
wa vitabu na Dr. Ntuyabaliwe Foundation, ikitanguliwa na Shule ya Msingi
 Hananasifu.
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja 
na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya 
Kinondoni wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la maktaba hiyo.
Mkurugenzi
 wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi alipowasili katika 
shule ya msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimkaribisha ofisini 
kwake Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi. 
Katikati ni Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyemwakilisha Afisa Elimu wa 
Wilaya ya Kinondoni katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi 
akibadilishana mawazo na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyekwamilisha 
Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni
 Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama 
Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule msingi Makumbusho 
kabla ya uzinduzi huo.
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimwongoza Mkurugenzi
 wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi kuelekea eneo la 
uzinduzi wa maktaba hiyo
  SHARE 
  









No comments:
Post a Comment