Korea Kaskazini
imedai kwamba kombora la masafara marefu ililolifanyia majaribio siku ya
Jumapili ni kombora jipya linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia .
Kombora
hilo lililorushwa lilienda anagani urefu wa kilomita 2,000 na kusafiri
kilomita 700 kabla ya kuanguka katika bahari Magharibi mwa Japan.Korea Kaskazini ilisema siku ya Jumatatu ni jaribio la uwezo wa kombora jipya.
Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa haliweza kuthibitisha madai hayo ya Korea Kaskazini.
- Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
- Trump: tutaidhibiti Korea Kaskazini
- Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa
Majaribio ya mara kwa mara ya makobora ya masafa marefu yanayofanywa na taifa hilo yanakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na yamesababisha wasiwasi miongoni mwa jamii ya kimataifa pamoja na Marekani.
Marekani na Japan zimetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.
Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema Jumatatu kwamba jaribio la kombora jipya la masafa marefu la Hwasong 12 lilifanyika kama ilivyopangwa.
Limesema kuwa jaribio hilo lililenga kuonyesha kwamba kombora hilo jipya lina uwezo wa kubeba kichwa cha Nyuklia.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment