TRA

TRA

Saturday, May 6, 2017

Macron adai kampeni yake imedukuliwa Ufaransa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Kamati ya kampeni ya mmoja wa mgombea wa urais nchini Ufaransa, Emmanuel Macron, imesema kuwa imevamiwa vikali na makundi ya udukuzi ambayo yamechapisha habari muhimu ya kundi lao katika mitandao ya kijamii.

Washiriki wa Bwana Macron wamesema kuwa barua pepe sahihi zimeibwa katika tarakilishi zao na kuchanganywa na zile bandia ili kuonyesha kuwa kamati hiyo ya Bwana Macron ni ya ubabaishaji tu. 


Mgombea wa urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron amedai kwamba wadukuzi waliidukua kampeni yake 

  
Chama cha Bwana Macron kijulikanacho nchini kama "En Marche" kilisema kuwa wachapishaji wa habari hizo zilizovurugwa wana nia ya kuvuruga demokrasia kabla ya uchaguzi wa marudio ya hapo kesho.

 Mpinzani mkuu wa Macron katika uchaguzi wa Urais nchini Ufaransa Marine Le Pen 

Tume ya Uchaguzi nchini Ufaransa inatarajiwa kuongoza mkutano wa dharura baadaye hii leo kujadili madai hayo ya udukuzi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger