Gazeti la New York
Times limeripoti kuwa China, imewauwa au kuwafunga jela majasusi kati ya
18 au 20 hivi wa CIA, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na
kulemaza kabisa shughuli za Marekani za kuichunguza China.
Polisi wa China wakilinda ubaloziu wa Marekani katika mji mkuu, Beijing
Baadhi ya watu sasa wanadhani kuwa China, ilidukua mfumo wa mawasiliano wa CIA, ambayo hutumiwa katika mazungumzo ya kisiri.
- China yarejesha chombo cha Marekani
- Ndege za China zazuia ndege ya Marekani
- Wakuu wa ujasusi Marekani kutoa ushahidi
Majasusi hao walianza kutoweka mmoja baada ya mwingine, kuanzia mwanzo wa 2011 (huku mmoja wao akipigwa risasi mbele ya wenzake katika eneo la kubarizi, kwenye jumba la serikali).
Idara ya ujasusi CIA, imekataa kuzungumzia swala hilo.
SHARE









No comments:
Post a Comment