Idara ya jeshi
nchini Marekani kwa mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la masafa
marefu lililo na uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi bara
lingine.
Mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani anasema iwapo miradi ya Korea Kaskazini ya kutengeneza makombora haitodhibitiwa, basi taifa hilo lina uwezo wa kutengeneza kombora lenye uwezo wa kufikia Marekani.
- Korea Kaskazini kutengeza kombora la masafa marefu
- Korea Kaskazini yalifanyia jaribio kombora la masafa marefu
- Marekani huenda isizuie makombora ya Korea
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa majaribio hayo yalipangwa mapema na kwamba haijibu kisa chochote.
Pentagon ilitangaza jaribio hilo wakati ambapo Korea kaskazini inatengeza kombora la masafa marefu.
Ni mara ya kwanza Marekani kujaribu kuzuia kudungua kombora la masafa marefu ICBM.
Marekani imekuwa ikitumia kifaa cha GMD kinachowekwa ardhini kukabiliana na mashambulio ya mataifa kama vile Korea Kaskazini.
Lina uwezo wa kudungua makombora mengine lakini hawajajaribu kudungua makombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
Huku maafisa wa Marekani wakiamini kwamba Pyongyang ina miaka mingi ya kuweza kufanikiwa kutengeza kombora la masafa, marefu ICBM , wanaamini taifa hilo limepiga hatua.
SHARE
No comments:
Post a Comment