Vyombo vya habari
nchini Brazil vinasema kuwa mifupa ya gwiji wa zamani wa soka nchini
humo Manuel Francisco dos Santos maarufu kama Garrincha, inaweza kuwa
imepotea zaidi ya miongo mitatu baada ya kifo chake akiwa na miaka 49.
Mmoja wa wahifadhi wa makaburi hayo anasma kuwa mifupa yake inaweza kuwa ilihamishwa miaka kadhaa iliyopita ila haijulikani wapi haswa ilipelekwa.
Garrincha mpinzani mkubwa wa Pele wa ni nani zaidi katika historia ya soka kwa nchi hiyo,aliisaidia nchi yake kutwaa kombe la dunia mwaka 1958 na 1962.
SHARE
No comments:
Post a Comment