Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Angellah Kairuki (kulia) akibadilishana mkataba wa ushirikiano wa
kuboresha sekta ya utumishi wa umma jimboni Puntland na Waziri wa
Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland Abdurahman Ahmed Abdulle, serikali
kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa kushirikiana na
Chuo kikuu cha Puntland itaendesha mafunzo hayo. Kushoto ni Makamu Mkuu
wa Chuo Kikuu Cha Puntland Mahmood Hamad.Hafla ilifanyika mwishoni mwa
wiki (Picha zote na Ino Communications)
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Angellah Kairuki (Kulia) na Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland
Abdurahman Ahmed Abdulle wakisaini mkataba wa Makubaliano ya
ushirikiano wa kuboresha sekta ya utumishi wa umma jimboni Puntland
ambapo serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)
itaendesha mafunzo hayo kwa kushiriakana na Chuo Kikuu cha Puntland.
Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Puntland Mahmood Hamad.
Mashauri
wa kisheria kutoka Puntland Burhan Adam Omar akijadili jambo kabla ya
kutia saini makubaliano baina ya Tanzania na Jimbo la Puntland
makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha sekta ya utumishi wa umma
jimboni Puntland ambapo serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania (TPSC) itaendesha mafunzo hayo kwa kushiriakana na Chuo Kikuu
cha Puntland.
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania katika hafla hiyo.
Picha
ya pamoja , katikati ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki, wa Kwanza kushoto ni
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Puntland Mahmood Hamad, wa Pili Kushoto ni
Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland Abdurahman Ahmed
Abdulle,Wanne kushoto ni Mkuu wa TPSC Dk. Henry Mambo na wa kwanza kulia
ni Mustapha Said Shaba Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma ya
Puntland.
SHARE
No comments:
Post a Comment