Na Sixmund J. Begashe
Serikali
ya Uswisi imeamua kuinga mkoni Serikali ya Jamhuuri ya Muungano wa
Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuziwezesha program tano
kiasi cha Dola za kimarekani 100,000 ambazo ni takribani Shilingi
milioni 220/= ili ziweze kutoa elimu kwa njia za burudani ya mapambano
dhidi rushwa nchini.
Akizungumza
kabla ya kusaini mikataba ya program hizo, Balozi wa Uswisi hapa nchini
Mh ARTHUR MATTLI amesema kuwa Tanzania kwa sasa inafanya vizuri zaidi
katika mapambano dhidi ya rushwa ukilinganisha na nchi nyingi barani
Afrika hivyo wameona ni vyema ikaungwa mkono katika mapambano haya.
Balozi
Mattli ameongeza kuwa hadi sasa takwimu zinaonesha kuwa katika nchi za
Afrika mashariki Tanzania inaongoza katika mafanikio yanayotokana na
mapambano dhiri ya rushwa hivyo serikali yake imeona nivyema ikaunga
mkono jitihada hizi kwa kuziwezeshwa program zitakazo toa elimu juu ya
madhara ya rushwa kwa kupitia sanaa ili watanzania waweze kuipokea
nakuielewa elimu hiyo kwa urahisi zaidi.
Akizungumza
baada ya kusaini makubaliano ya kupokea fedha za kuendesha programa ya
Museum Art Explosion, kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw
Saimon Maliti pamoja na kuishukuru Serikali ya Uswizi kwa kutambua
jitihada za Makumbusho ya Taifa katika kuelimisha jamii juu ya mambo
yanayo wahusu, amemwakikishia Balozi huyo kuwa fedha walizo pata
zitatumika kama zilivyo kusudiwa na si vinginevyo.
Nae
Mkurugenzi wa Elimu kwa Jamii wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa nchini (TAKUKURU) Bw EKWABI MUJUNGU ameishukuru Serikali ya
Uswizi kwa kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya
Rushwa na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na Taasisi zilizo wezeshwa na
Ubalozi huo ili kuhakikisha malengo yaliyokusudia ya kupambana na rushwa
yanafanikiwa.
Taasisi
zilizo wezeshwa ni pamoja Makumbusho ya Taifa kupitia Program ya MUSEUM
ART EXPLOSION AGAINST CORRUPTION, Tanzania House of Talent (THT),
Kijiji Studii Tanzania, Goba Africa LTD na Art in Tanzania.
Katikati
ni Balozi wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa
program zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa
nchini.
Balozi
wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa program
zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Katikati ni Balozi wa Uswisi nchini Mh ARTHUR MATTLI na
kulia ni Mkurugenzi wa Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles
Bufure wakishuhudia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw
Saimon Maliti akitia sahii makubaliano ya fedha za kuendeshea program ya
Museum Art Explosion kwa mapambano dhidi ya rushwa
Kulia
ni Mkurugenzi wa Elimu kwa Jamii wa TAKUKURU Ekwabi Mujungu na
Muanzilishi wa THT Bw Ruge Mutahaba wakimsikiliza kwa Makini Balozi wa
Uswisi nchini Mh ARTHUR MATTLI(hayupo pichani)
SHARE
No comments:
Post a Comment