Abiria wanaosafiri na Shirika la Ndege la British Airways, wamecheleweshwa kwa sababu ya matatizo ya kompyuta.
Baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa matatizo hayo huenda yameathiri shughuli za shirika hilo dunia nzima.BA imeomba msamaha katika mitandao ya jamii, na inasema inajaribu kumaliza tatizo hilo haraka iwezekanavyo.
- China yazindua meli kubwa ya kivita
- Ndege ya kwanza iliyoundwa China yapaa
- Tanzania kununua ndege mpya ya Boeing
Ndege za kampuni hiyo zinazotua katika uwanja wa Heathrow mjini London haziwezi kuegeshwa kwa kuwa ndege zinazoondoka haziwezi kutoka katika lango kuu, hali iliowafanya abiria kukwama katika ndege.
Mwandishi Martyn Kent alisema kuwa amekuwa ndani ya ndege katika uwanja wa Heathrow kwa dakika 90.
Anasema kwamba rubani wa ndege aliambia abiria kwamba tatizo hilo la kompyuta ni 'janga'.
Uwanja wa ndege wa Heathrow umewashauri abiria kuangalia muda wa safari zao kabla ya kuelekea katika uwanja huo
SHARE
No comments:
Post a Comment