• About
  • Services
  • Products
  • Blog
  • Contact Us

NCHI YANGU

Menu
  • Home
  • Lifestyle
    • Sub Menu 1
    • Sub Menu 2
    • Sub Menu 3
  • Sports
    • Sub Menu 1
      • Sub Menu 1
      • Sub Menu 2
      • Sub Menu 3
    • Sub Menu 2
    • Sub Menu 3
  • Post
  • Fitness
  • Music
  • Travel
  • Politics
  • Beauty

TRA

TRA

Wednesday, May 24, 2017

Home > > TTB: Tembeleeni vivutio vya utalii

TTB: Tembeleeni vivutio vya utalii

at 4:03 AM
Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imetoa wito kwa Watanzania kupenda kutembelea vivutio vya utalii vya ndani kwa lengo la kukuza na kuinua pato la Taifa.

Wito huo ulitolewa jana na Ofisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii, Geofrey Tengeneza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya kuhusiana na kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani iliyozinduliwa mkoani Mbeya.

Tengeneza alisema Bodi ya Utalii ilifanya utafiti mwaka 2006 na kubaini kuwa idadi kubwa ya Watanzania hawatembelei vivutio vya Utalii vya ndani na badala yake wanajua kazi ya Utalii ni ya wageni kutoka nje ya Nchi.

Alisema baada ya kugundua uwepo wa changamoto hiyo Bodi ilianzisha kampeni mbali mbali za kuhamasisha utalii wa ndani mwaka 2007 ambapo idadi ilianza kuongezeka kutoka watalii 250,000 hadi zaidi ya 800,000 sasa.



Geofrey Tengeneza
Twiga

Alisema matarajio ya Bodi ni kuona utalii wa ndani unaingiza pato kubwa kwa Taifa bila kutegemea Utalii wa Kimataifa hivyo kuendelea kuendesha kampeni zingine zaidi.

Alisema kutokana na kuonekana Wananchi bado wanahitaji elimu zaidi kuhamasishwa kutembelea vivutio vya utalii vya ndani Mei 3, mwaka huu Bodi ilizindua kampeni mpya.

Aliitaja kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa katika Mkoa wa Kigoma na kuendelea katika mikoa minne kuwa ni “Utalii wa ndani uanze na mtanzania mwenyewe”.

Aliongeza kuwa baada ya kuzindua kampeni hiyo mkoani Kigoma Bodi ilizindua tena katika Mkoa wa Iringa na sasa Mbeya kisha Mkoa wa Mwanza.

Akizungumzia uzinduzi wa kampeni hiyo katika Mkoa wa Mbeya alisema itafanyika katika viwanja vya Uhasibu kuanzia majira ya saa moja jioni ambapo Agape Television Network(ATN) itakuwa ikionesha matukio ya utalii kupitia skrini kubwa.

Aidha alitoa wito kwa mashirika binafsi kujitokeza katika kuwekeza kwenye miundombinu ya malazi kwenye maeneo yenye vivutio vya Utalii ili kuwavutia watu wanaotembelea.

Alisema kupitia kampeni hiyo mashindano mbali mbali yataendeshwa ambapo washindi watapelekwa kwenye hifadhi za Taifa kutembelea ikiwemo kujishindia zawadi mbalimbali. 

Habari hii imendaliwa na Venance Matinya




Unknown

Author: Unknown

SHARE
  • Share
  • Tweet
  • Share
  • Pin
  • Share
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Fourni par Blogger CodeEnvoyer par emailBlogThis !Partager sur TwitterPartager sur FacebookPartager sur LinkedInÉpingler sur PinterestPartager sur StumbleUponVoter pour cet article sur HelloCoton

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Tupate kupitia Facebook

Popular Posts

  • Vyuo vikuu bora zaidi duniani mwaka 2017
    ...
  • WAUMINI WA ASKOFU GWAJIMA WACHANGIA DAMU MUHIMBILI
    W...
  • Afande Sele na uvutaji bangi
    Afande Sele Aungana Na Mbunge Joseph Msukuma Kuitaka Serikali Ihalalishe Matumizi Ya Bhangi

Popular Posts

  • Vyuo vikuu bora zaidi duniani mwaka 2017
    Vyuo vikuu bora zaidi duniani mwaka 2017
    ...
  • WAUMINI WA ASKOFU GWAJIMA WACHANGIA DAMU MUHIMBILI
    W...
  • Afande Sele na uvutaji bangi
    Afande Sele Aungana Na Mbunge Joseph Msukuma Kuitaka Serikali Ihalalishe Matumizi Ya Bhangi
  • TANAPA WAFUNGUA OFISI JIJINI DAR ES SALAAM
    TANAPA WAFUNGUA OFISI JIJINI DAR ES SALAAM
     Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya TANA...
  • PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 7,2017
    PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 7,2017
  • WANARIADHA WAPONGEZWA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA JIJINI DAR
    WANARIADHA WAPONGEZWA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA JIJINI DAR
    Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa, Meja jenerali, Michael Isamuhyo akizungumza wakati wa kumpongeza Mshindi wa tatu wa Mbio za Dunia za...

Pages

  • Home
  • About Us
  • Contat Us
 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger