Na Mwamvua Mwinyi ,Chalinze
Mbunge wa jimbo la
Chalinze, Ridhiwani Kikwete ,amekemea wanaodhihaki utendaji kazi wa Rais Dk.John Magufuli na kudai anakonga nyoyo za wananchi wanyonge kwa
kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.
Amesema haoni aibu
kumuunga mkono rais,na Chalinze inaendelea kutamba kwa hatua mbalimbali
za kimaendeleo na kiuchumi zinazochukuliwa.
Aidha Ridhiwani
hakusita ,kutoa kilio cha maji licha ya serikali na Chaliwasa kupambana
ili kuondoa tatizo hilo kwa wanaChalinze .
Akizungumza katika
ziara ya rais dk .Magufuli aliyoifanya Bagamoyo ,mbunge huyo alisema
,anaipongeza serikali na yeye anaendelea kusimamia kero zote ili
kuhakikisha Chalinze inapiga hatua na kuwa katika sura mpya .
Alisema hatokuwa nyuma kuiunga mkono katika hatua zinazochukuliwa ikiwemo kupambana na Ufisadi .
“Kama yupo mtu
mwenye shaka na utayari wako na uchapakazi wako juu ya sera ya viwanda
basi aje Chalinze kuona maendeleo yaliyopo ,na tunatamba kwa hilo.”
Tunajua wewe ni kazi tu na sisi hapa chalinze ni kazi tu. “
Ridhiwani alisema
,tatizo la maji bado ni kubwa hivyo ameiomba serikali ione umuhimu wa
kushirikiana na wawekezaji wanaojitoa kusaidia changamoto hiyo .
“Alimpongeza Subash
Patel na mwekezaji kampuni ya vigae Twyford kilichopo Pingo kwa
kuonyesha nia yao kusaidia tatizo la maji ” aliongeza Ridhiwani .
Ridhiwani alibainisha halmashauri yao inaongoza kwa makusanyo ya mapato ya ndani kwa asilimia 102 .
“Mh. Raisi ,
tumejipanga halmashauri yetu inajiwezesha yenyewe.Zaidi ya Milioni 200
zimepelekwa kuwezesha vikundi vya ujasiriamali katika mikopo ya vijana
na wanawake.
Ridhiwani anashirikiana vyema na halmashauri hiyo ,na ameshasaidia ujenzi wa shule ya Moreto iliyowahi kuungua.
Pia alishatoa gari la wagonjwa,vitanda katika shule za msingi na sekondari jimboni hapo ,vitabu vya kujifunzia kwa shule hizo.
Ridhiwani aliwahi
kutoa mabati na mifuko ya saruji vilivyogharimu mamilioni ya fedha
katika ujenzi wa baadhi ya madarasa ,zahanati ,na ofisi mbalimbali za
mashuleni na vijiji .
Nae Mkuu wa mkoa wa
Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,alikumbushia halmashauri ya Chalinze
,kupewa majengo yaliyokuwa yakitumika na mkandarasi aliyekuwa akijenga
barabara ya Msata -Chalinze .
Rais Magufuli aliuambia umati uliokuwepo katika shughuli hiyo kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka.
Alisema ni hakika Ridhiwani anaonyesha uwezo wa kiuongozi na sio kama kachaguliwa kwa mgongo wa mtu .
Dk.Magufuli
alimfananisha Riz na Baba yake dk.Kikwete aliyewahi kuwa raisi Wa
Jamhuri ya Tanzania wakati wa awamu ya Nne na kusema kweli kaya hiyo ni
ya wanasiasa .
Mbali na hayo
aliikabidhi halmashauri ya Chalinze majengo ambayo yalitumiwa na
Mkandarasi Wa barabara ya Msata wakati wa Ujenzi wa Barabara ya
Bagamoyo-Makofia-Msata.
Alieleza anatoa
majengo hayo bure na halmashauri hiyo itajipangia matumizi yake na
kuiomba itunze mali zilizomo kwenye majengo hayo.
WAKATI HUO HUO ,mkuu
Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Ndikilo alimshukuru rais Dk.Magufuli kwa
kufanya ziara ya siku tatu Mkoani hapo .
Alieleza ,kwa hakika
wananchi wamefarijika kwa mikutano aliyozungumza nao
,kukagua,kutembelea kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi ya
kiuchumi na kimaendeleo ikiwa ni sanjali na miundombinu ya barabara,maji
na uwekezaji ,kuanzia june 20 hadi June 22 .
Mhandisi Ndikilo
,alielezea kwamba,wananchi walio wengi watakuwa wamejua namna serikali
yao inavyofanya kazi kwa manufaa ya Taifa na mkoa .
Kwa upande wa wananchi wa wilaya ya Kibaha na Bagamoyo ,walimshukuru dk.Magufuli kwa kuwatembelea na kufuturu nao pamoja .
Mgeni Msafiri
,alisema hakika wamefarijika na ziara hiyo na wamepokea yale
aliyoyasisitiza kwa jamii ikiwemo kusomesha watoto hasa Wa kike kwa
manufaa yao baadae .
“Alituhimiza pia kufanya kazi ,kuacha uvivu na kutumia viwanda vilivyojengwa Mkoani kwetu ” alisema Mgeni.
Jesca Mingo ,alisema haijawahi kutokea kwa miaka mingi rais kulala ikulu ndogo ya Mkoa Wa Pwani .
SHARE








No comments:
Post a Comment