Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu
anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana amefungua mpango wa
mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa kwa
vijana 1000 wanaotaka mikoa zaidi ya kumi nchini.
Akizundua mpango huo, Mhe Mavunde, amesema mpango huo unalenga
kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana na pia kutumia bidhaa zitokanazo na
mazao ya mifugo kwa ajili ya kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi nchini.
Amesema, serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe
Magufuli imejipanga kuhakikisha inatekeleza azma ya ujenzi wa viwanda
kwa kuwajengea uwezo vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa katika
kujiandaa na mfumo wa mapinduzi ya viwanda ambavyo vimeshaanza kujengwa
nchini.
Aidha amewataka vijana kutochagua kazi au kubweteka kuwa kazi
rasmi ni zile za ajira ya moja kwa moja serikali au sekta binafsi,
amewataka vijana kubadilisha mtazamo wa maaana ya Ajira kwa kutokukaa na
kusubiri nafasi za ajira.
Amesema mpango huu wa miaka mitano unalenga kuwafikia vijana
zaidi ya milioni 4 nchini katika kuwajengea uwezo ambao utawafanya
kujiajiri au kuajiriwa katika Tanzania ya viwanda.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano.
Wizara ya kazi,ajira, ulemavu na maendeleo ya vijana
03/06/2017
SHARE
No comments:
Post a Comment