Mshambuliaji wa
Tottenham Clinton Njie anatarajiwa kujiunga na klabu ya Marseille ya
Ufaransa kwa mkataba wa kudumu baada ya klabu hizo kuafikiana.
Njie alijiunga na Spurs kutoka Lyon mwaka 2015 kwa £10m na kuchezea klabu hiyo mechi 14, ingawa aliumia kwenye goti Desemba 2015.
"Tunamtakia Clinton kila la kheri siku zake za baadaye," Tottenham wamesema.
SHARE
No comments:
Post a Comment