Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua chumba cha upasuaji kilichopo katika moja ya kituo cha Afya wilayani Ukerewe.
Akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo, Jafo amefika kwenye hospitali ya wilaya ya ukerewe na kuwaomba wananchi waliokuwepo hospitalini hapo kueleza changamoto wanazozipata wanapofika hospitalini hapo.
Kufuatia changamoto walizoeleza wananchi, Jafo alionyesha kukerwa kutokana na maafisa hao kushindwa kujibu hoja ya wananchi waliokuwa wakilalamika kwamba wanapofika kwenye hospitali hiyo mara nyingi wataalam wamekuwa na kauli mbaya sambasamba na kukosa dawa.
Jafo aliwageukia wataalam hao kwa kuwauliza ni kiasi gani cha fedha za basket fund wamepokea kwa mwaka Fedha 2016/2017 na kiasi gani kilitumika kununua dawa na vifaa tiba.
Kutokana na Jafo kuhoji fedha hizo, wataalam hao wote walishindwa kufahamu, jambo lililomkera Naibu Waziri Jafo.
Alisema ameshangazwa na kitendo cha wataalam wahusika kushindwa kutambua mambo ya msingi ambayo wanapaswa kuyasimamia ili kutatua kero ya afya kwa wananchi.
Jafo aliwajulisha wananchi kuwa halmashauri yao imepokea jumla ya sh.milioni 727.4 ambapo 33% ilipaswa kununulia dawa na vifaa tiba.
Naibu Waziri Jafo amewataka watumishi wote kusimamia mipango ya serikali ili kutatua kero za wananchi ili kuleta maendeleo katika jamii.
SHARE









No comments:
Post a Comment