Muadhama
Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam
akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Prof. Mohamed Janabi leo muda mfupi kabla ya kuanza kwa sherehe
kutimiza miaka 25 kama kiongozi wa Kiroho katika kanisa la Katoliki
jimbo Kuu la Dar es salaam katika kanisa la St. Joseph.
Muadhama
Polycarp Kardinali Pengo ni kardinali wa pili kutoka Tanzania, akiwa
kateuliwa mara baada ya kifo cha Muadhama Laurean Rugambwa, aliyekuwa
kardinali wa kwanza kutoka kusini kwa Sahara.
Alizaliwa
kijiji cha Mwazye, mkoani wa Rukwa, tarehe 5 Agosti 1944. Baada ya
masomo ya ngazi mbalimbali, alipewa upadrisho mwaka 1971 na askofu
Charles Msakila wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga, akasoma teolojia ya
maadili huko Roma, Italia, akijitwalia digrii ya udaktari mwaka 1977.
Kisha kufundisha somo hilo kwa muda mfupi kwenye seminari kuu ya Kipalapala (mkoa wa Tabora), baadaye
Kisha kufundisha somo hilo kwa muda mfupi kwenye seminari kuu ya Kipalapala (mkoa wa Tabora), baadaye
alichaguliwa kuwa gombera wa seminari kuu ya Segerea hadi mwaka 1983.
Aliteuliwa
askofu wa Nachingwea tarehe 11 Novemba 1983, akapewa daraja takatifu
hiyo na Papa Yohane Paulo II tarehe 6 Januari 1984.
Tarehe
17 Oktoba 1986 alihamishiwa jimbo jipya la Tunduru-Masasi.
Tarehe 22 Januari 1990 alifanywa askofu mwandamizi wa Dar-es-Salaam na
mwaka 1992, ambapo Kardinali Laurean Rugambwa alipojiuzulu, akawa askofu
mkuu.
Muadhama
Polycarp Kardinali Pengo aliteuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa
kardinali tarehe 21 Februari 1998, akikabidhiwa parokia ya Nostra
Signora de La Salette mjini Roma.
Pamoja
na majukumu mbalimbali katika idara za Papa, tangu mwaka 2007 hadi 2013
alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika
na Madagaska.
SHARE
No comments:
Post a Comment