TRA

TRA

Friday, July 7, 2017

Arsenal yazidi kuchukua vifaa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alexandre Lacazette toka timu ya Lyon kwa dau la pauni Milioni 52.6 na kuvunja rekodi ya usajili ya timu hiyo.

Usajili wa kiungo wa Kijerumani Mesut Ozil ndio ulikua usajili wa bei ghali zaidi klabuni hapo aliposajiliwa mwaka 2013, kutokea Real Madrid kwa dau la pauni 42.4.
 Alexandre Lacazette

Lacazette amesaini mkataba wa miaka mitano kuwatumikia washika mitutu hao wa London (Arsenal), mshambuliaji huyu atasafiri na timu wikiendi hii kuelekea Sydney kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki.


Msimu uliopita, Lacazette alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Ufaransa alikozipasia nyavu mara 28 na ameshapiga jumla ya mabao 129 katika mechi 275 tangu alipoanza kuichezea timu ya kwanza msimu wa 2009/10.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger