Uzinduzi wa albamu ya tatu
kutoka kwaya ya JERUSALEM CITY SINGERS ya Bugarika Jijini Mwanza,
unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo Julai 23,2017 katika viunga vya
Rock/ Kishimba Beach Garden Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa kwaya hiyo, Samwel
Maneno amesema hakuna kiingilio katika uzinduzi huo na kwamba shughuli
nzima itaanza majira ya saa saba kamili mchana ambapo waimbaji
mbalimbali wakiwemo Born To Praise, Voice Of Calvary na Lake Zone
watahudumu siku hiyo.
“Hii ni albamu yetu ya tatu ya
video iitwayo MUNGU WA AJABU ambapo imetanguliwa na albamu mbili ambazo
ni DUNIA MAHUTUTI na HAJAKUSAHAU hivyo nawakaribisha watu wote kushiriki
nasi kwenye uzinduzi huo”. Amesema Maneno.
Bonyeza HAPA taarifa zaidi
SHARE
No comments:
Post a Comment