Bunge la Iran limepitisha mswada wa kutenga zaidi ya dola nusu bilioni zaidi, kwa ajili ya mradi wa makombora.
Iran inajibu vikwazo vya karibuni kabisa, vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi hiyo.
Vyombo vya habari vya taifa, vinasema, fedha hizo zinakusudiwa kupambana
na vile vilivoitwa, vitendo vya kigaidi vya Marekani katika Mashariki
ya Kati.
Mswada huo utaweka vikwazo dhidi ya wanajeshi pamoja na maafisa wa ujasusi wa Marekani.
Mpatanishi mkuu wa Iran katika mazungumzo kuhusu mradi wake wa nuklia,
Abbas Araqchi, amesema, mswada huo mpya, umeungwa mkono na wizara ya
mashauri ya nchi za nje, na kwamba hauendi kinyume na makubaliano ya
mwaka 2015, yaliyozuia mradi wa nuklia wa Iran.
Makubaliano kuhusu programu ya nuklia kati ya Iran na mataifa sita yenye
nguvu duniani ikiwemo China, Urusi na Uingereza,, yanaonekana kwa
kiwango kikubwa kama njia mwafaka ya kuizuia Iran kuunda zana za nuklia.
Makubaliano hayo yalisababisha vikwazo vibaya kwa uchumi wa Iran
kuondolewa, ili nchi hiyo ipate kupunguza programu zake za nuklia.
SHARE
No comments:
Post a Comment