TRA

TRA

Monday, August 14, 2017

Jeshi la Uganda lasema halina mpango wa kuingia Kenya

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Jeshi la Uganda

Jeshi la Uganda Jeshi la Uganda la UPDF limekanusha taarifa kuwa liko tayari kuingia nchini Kenya kusaidia kudhibiti hali ya usalama nchini humo baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, huku mpinzani wake mkuu Raila Odinga akiyapinga matokeo hayo.

Waziri wa mawasiliano nchini humo, Frank Tumwebaze amesema Jeshi la Uganda haliwezi kutumwa nje kushiriki operesheni ya kijeshi kisiri.

Msemaji wa jeshi la Uganda Richard Karemire, kupitia taarifa, amesema Kenya ni nchi huru na usalama wake umo chini ya serikali ya nchi hiyo.

Aidha, amesema Uganda haijapokea ombi kutoka kwa Kenya kutuma majeshi yake nchini humo au kuomba usaidizi.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger