![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjYzUOArXuv7KZiPFl8J8V_T-0insMX6KWEyQ8lt6bodzeHCi85-1k6phszLAwMDDV1eqPfKApNf2rTV5MRF4zWm3MZvjRK8DraRlnqFRfD-MeJoBabFNDAtE6JsdLZrImxmDs56o4VW4g/s640/1.jpg)
Nyumba za kifahari zilizojengwa pembezoni maeneo ya Kimara mpaka Kiluvya
jijini Dar es salaam zimekumbwa na bomoabomoa kitu ambacho kimeumiza
watu wengi sana, kwani wapo ambao hawana makazi na hawaelewi nyumba zao
zikibomolewa wataanzia wapii na wataishi wapi.
Na nyumba ya Mbunge wa Mikumi ni moja ya nyumba ambazo zimewekewa X kuashiria nayo imo miongoni mwa nyumba za kubomolewa.
Hivi karibuni Tanroads imetangaza kuwa muda wowote itaanza utekelezaji
wa kubomoa nyumba zilizowekewa alama ya X katika barabara hiyo kupisha
ujenzi wa barabara kubwa ya kisasa.
Tayari Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza kukata umeme kwenye
nyumba nyingi hivyo kuwafanya baadhi ya wenye nyumba kubomoa wenyewe
kwa hiari na kufungasha mizigo yao.
Tazama picha ya nyumba ya kifahari ya mbunge wa Chadema Joseph Haule
maarufu kama Profesa jay ambaye hivi karibuni alifunga harusi kubwa na
kuweka jiko ndani.
SHARE
No comments:
Post a Comment