Idara ya Uhamiaji inapenda
kuufahamisha Umma kwamba, utolewaji wa pasipoti zenye hadhi ya
Kidiplomasia (Diplomatic Passport) na Kiutumishi (Service Passport) upo
kwa mujibu wa Sheria ya Pasipoti na Hati za Kusafiria Sura ya 42 ya
mwaka 2002 pamoja na Kanuni zake.
Katika Vifungu Namba 10(2) na
(3) na Jedwali la Pili na la Tatu la Sheria hiyo, makundi mbalimbali ya
watu wanaostahiki kupewa pasipoti hizo yameainishwa.
Hivyo, Idara ya Uhamiaji
inawataka wale wote ambao wamefikia ukomo wa Utumishi wa nyadhifa na
hadhi hizo, warejeshe pasipoti hizo kwenye Ofisi za Uhamiaji ndani ya
kipindi cha mwezi mmoja tangu tarehe ya kutolewa kwa taarifa hii, kama
yalivyo matakwa ya Kifungu cha 8(2) cha Sheria tajwa hapo juu; isipokuwa
wale ambao kwa mujibu wa nyadhifa zao wanaruhusiwa kisheria kuendelea
kutumia Pasipoti hizo hata baada ya kustaafu kwao wakiwemo Viongozi
Wakuu wa Nchi wastaafu, Wakuu wa Mihimili ya dola Wastaafu na Wakuu wa
Vyombo vya Ulinzi na Usalama Wastaafu kama ilivyoainishwa katika Jedwali
la Tatu kwenye Sheria hiyo.
Baada ya kuisha kwa kipindi
tajwa yaani mwezi mmoja baada ya kutolewa kwa taarifa hii, wasiostahiki
kuwa nazo watazuiliwa safari zao mara watakapopita katika vituo vya
kuingia na kutoka nchini ikiwa ni pamoja na Viwanja vya Ndege. Aidha,
ieleweke kwamba, kuendelea kuwa na Pasipoti hizo kwa wasiostahiki ni
kosa kisheria chini ya kifungu cha 19(2)(k) cha Sheria tajwa.
Imetolewa na
KITENGO CHA UHUSIANO,
IDARA YA UHAMIAJI,
MAKAO MAKUU.
15 AGOSTI, 2017.
SHARE
No comments:
Post a Comment